NLD YAWASHUKURU WANANCHI TANZANIA BARA NA ZANZIBAR - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, August 22, 2025

NLD YAWASHUKURU WANANCHI TANZANIA BARA NA ZANZIBAR


NA MWANDISHI WETU

CHAMA cha National League for Democracy (NLD) kinapenda kutoa shukrani za dhati kwa wananchi wote waliokijitokeza kwa wingi katika mikoa 10 ya Tanzania Bara na Zanzibar kwa ajili ya kumdhamini mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho.


Katika taarifa  iliyotolewa na chama hicho Leo, imesema mchakato wa upatikanaji wa wadhamini ulianza rasmi Agosti 10, 2025, mara baada ya Doyo Hassan Doyo, mgombea wa Urais kupitia NLD, kuchukua fomu ya uteuzi.

Imesema  mchakato huo umehitimishwa rasmi leo, Agosti 22, 2025,  jijini Dar es Salaam kutokana na kiapo cha mgombea huyo katika Mahakama Kuu ya Tanzania ni hatua muhimu inayomwezesha kukidhi vigezo vya kuendelea na mchakato wa uteuzi.


"Mgombea wetu anatarajia kurudisha fomu ya uteuzi rasmi tarehe 24 Agosti 2025, jijini Dodoma, na kisha kusubiri uamuzi na uteuzi rasmi kutoka Tume Huru ya Uchaguzi.


"Tunatambua kwa dhati na kuthamini moyo wa uzalendo, mshikamano na imani mliyoonesha katika hatua hii muhimu ya kisiasa kwa chama chetu na kwa taifa kwa ujumla. 

"NLD itaendelea kusimama imara kwa ajili ya maslahi ya wananchi na maendeleo ya kweli ya Tanzania", imesema.


No comments:

Post a Comment