Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi ametembelea Banda la Wakala wa Vipimo (WMA) katika Maonesho ya NaneNane Dodoma na kuwapongeza watendaji wake kwa kazi nzuri wanayoifanya.Mhe. Kabudi amesema WMA ni miongoni mwa Taasisi muhimu za Serikali zinazogusa maisha ya wananchi moja kwa moja.
Ametoa rai kwa watendaji wa WMA kuendelea kuchapa kazi kwa bidii ili kuwalinda walaji katika sekta zote nchini wakiwemo wakulima kupitia jukumu lao kuu la uhakiki wa vipimo.
No comments:
Post a Comment