NA MWANDISHI WETU
KATUBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema kesho, Agosti 12, 2025 watazindua harambe yenye lengo la kukusanya Shilingi Billion 100 zitakazotumika kwenye shughuli ya kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.
Dkt Nchimbi amesema hayo leo, Agosti 11, 2025 katika Ofisi Ndogo Makao Makuu, Lumumba jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya Habari.
"Harambee ya kuchangia kampeni za chama itakazinduliwa rasmi kesho katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na inalenga kukusanya Shilingi Bilioni 100 kwa ajili ya maandalizi ya kampeni, ikiwemo gharama za magari, mabango, mafuta, fulana na kanga," amesema.
![]() |






No comments:
Post a Comment