WALIOONGOZA KURA ZA MAONI CCM WASIFANYE KAMPENI HADI UTEUZI - MRAMBA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, August 15, 2025

WALIOONGOZA KURA ZA MAONI CCM WASIFANYE KAMPENI HADI UTEUZI - MRAMBA


NA MWANDISHI WETU, PWANI 

WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani waliowania nafasi za Ubunge na Udiwani na kuongoza kwenye kura za maoni hawapaswi kuanza kufanya kampeni hadi majina yao yatakapotangazwa rasmi.


Hayo yamesemwa Mjini Kibaha na Katibu wa Siasa Uenenzi na Mafunzo Mkoa wa Pwani David Mramba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo majina hayo yaliyopendekezwa yatapelekwa Taifa kwa ajili ya kutangazwa baada ya vikao vya Sekretarieti ya halmashauri Kuu ya CCM Taifa.


Mramba amesema kuwa walioongoza watakiwa wasubiri hatma yao baada ya vikao vya juu badala ya kujiona kuwa tayari wameshashinda nafasi hizo na kuwa wagombea kupitia chama hicho hawapaswi kufanya sherehe au kampeni hadi pale majina yao yatakapotangazwa na makao Makuu lakini kwa sasa siyo washindi bali waliongoza tu.


"Natoa rai kwa wale wote walioongoza kwenye kura za maoni ya Ubunge na Udiwani bado hawajateuliwa hadi pale majina yao yatakapotangazwa wasifanye shughuli yoyote inayohusiana na kampeni hadi hapo majina hayo yatakapotangaazwa rasmina CCM Taifa na kurejeshwa kwetu na kuyatangaza rasmindipo waendelee na kampeni"amesema Mramba.


Amesema kuwa baada ya uchaguzi vikao vimekaa kuanzia ngazi ya Kata Wilaya na Mkoa na Halmashauri Kuu ya CCM ilikaa pamojana kikao hicho kilijadili majina ya wabunge na madiwani na kura walizopata na uteuezi wa majina ya Madiwani wa Viti Maalum na Kata.


No comments:

Post a Comment