JAJI MWAMBEGELE APOKEA TAARIFA YA MAJIMBO YA MTERA NA CHAMWINO MKOANI DODOMA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, September 25, 2025

JAJI MWAMBEGELE APOKEA TAARIFA YA MAJIMBO YA MTERA NA CHAMWINO MKOANI DODOMA


Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele leo Septemba 25, 2025 ametembelea  Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma  katika majimbo ya Chamwino na Mtera ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 ambapo pamoja na mambo mengine alipokea taarifa ya majimbo hayo kutoka kwa msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri kuhusu maandalizi ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2025 na kisha kukagua vifaa ambavyo tayari vimepokelewa katika Halmashauri hiyo.  

Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa na Tume, Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 unatarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.

"Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura"





No comments:

Post a Comment