MGOMBEA UBUNGE KIGAMBONI KWA TIKETI YA CUF KUIBURUZA SERIKALI MAHAKAMANI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, October 8, 2025

MGOMBEA UBUNGE KIGAMBONI KWA TIKETI YA CUF KUIBURUZA SERIKALI MAHAKAMANI

 

NA MWANDISHI WETU

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Kigamboni kupitia Chama Cha Wananchi (CUF), Mohamed Majaliwa amedai kwamba tayari amefungua kesi mahakamani kwaajili ya kutaka maelezo ya Serikali sababu ya wanaotumia Daraja la Kigamboni kulipa ushuru wakati mengine yanatumika bure.

Majaliwa ambaye pia ni Mwanasheria ametanabaisha hayo Oktoba 5, 2025 wakati akinadi sera zake kwa wananchi wa Buyuni, Kata ya Pemba Mnazi, Kigamboni jijini Dar es Salaam na kufafanua kwamba haiwezekana Daraja la Busisi, Wami na Tanzanite yapitike bure halafu Kigamboni walipe.

“Tayari tumefungua kesi kuhusu daraja la Kigamboni na wiki ijayo mtaanza kuisikia kupitia Vyombo vya Habarii mbalimbali, tunahiita Serikali mahakamani ije ituambie tumewakosea nini kutupa ile adhabu pale, Serikali ni wajibu wake ni kukusanya mapato na kutungeneza daraja ili wananchi wapite bure,” amesema.

Amefafanua kuwa anaamini wananchi hao tayari wametimiza wajibu wao kwa kulipa kodi kupitia bidhaa mbalimbali wanaonunua kwa ajili ya mahitaji yao ya kila siku na kinachotahitajika kwa sasa ni Serikali kuhakikisha inatekeleza wajibu wake kwa kuruhusu Daraja la Kigamboni linapitika bure bila malipo na si kuwabebesha masalaba wananchi.

Kada huyo Chama Cha Cuf, amesema haiwezekani hadi sasa wanaopita katika daraja hilo waendelee kutozwa ushuru na kuhoji ni lini Serikali ilikaa na wananchi wa Kigamboni na kukubaliana ulipaji ushuru na tangu ulipaji huo uanze hadi sasa ni kiasi tayari kimekusanywa na kilichobaki ili kijulikane.

Amefafanua kwamba uwezo wa kubeba suala hilo anao kwa maslahi ya wanatumiaji wa daraja hilo na wakazi wa Kigamboni, hivyo amewaomba wananchi hao kuhakikisha wanakipigia kura kwa wingi Chama Cha Cuf ili kuiondoe kero hiyo.

Pia ameongeza kuwa mchakato mwingine ambao wataufanya ikiwa Cuf itachukua Jimbo hilo, watahakikisha wananunua magari ya Zimamoto kwa kuwashirikisha wawekezaji waliomo jimboni humo  ili kurahisisha uzimaji moto kwa haraka  ikiwa janga la aina hiyo litatokea.

Kuhusu shughuli za uvuvi zilizopo katika eneo la Buyuni, Majaliwa aliahidi kuwa ikiwa atachaguliwa kuwa Mbunge atahakikisha linajengwa soko kubwa la samaki litakalokuwa na majokofu ya kuhifadhia mavuno hayo ya bahari pamoja na kujengwa maduka yatakayouza zana za wavuvi.

 

 

 

 









No comments:

Post a Comment