TAMASHA LA NYAMAPORI CHOMA LAVUTA UMATI TABORA ZOO - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, October 18, 2025

TAMASHA LA NYAMAPORI CHOMA LAVUTA UMATI TABORA ZOO


NA MWANDISHI WETU, TABORA

ZAIDI ya watalii 500 wamefurika leo, Oktoba 18, 2025, katika Bustani ya Wanyamapori Tabora (Tabora Zoo) kushiriki katika Tamasha la Nyamapori Choma lililoandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Kanda ya Magharibi.


Tamasha hilo lililolenga kuhamasisha utalii wa ndani pamoja na matumizi endelevu na halali ya rasilimali za wanyamapori, limevutia watalii  kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi, likihudhuriwa na viongozi wa Serikali wakiwemo Wakuu wa Wilaya za Tabora na Uyui, wananchi wa Mkoa wa Tabora na mikoa jirani, pamoja na wageni kutoka mataifa mbalimbali duniani.


Wananchi waliohudhuria tamasha hilo wameipongeza TAWA kwa ubunifu wa kuandaa tukio hilo, wakieleza kuwa limewapa fursa ya “kuonja ladha ya matunda ya uhifadhi” unaotekelezwa na Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii Kwa kuhakikisha wananchi wananufaika na rasilimali hizo Kwa njia halali bila kuathiri uhifadhi endelevu.


Kwa siku nzima ya leo, anga la Tabora Zoo lilitawaliwa na nderemo, shamrashamra za muziki wa asili, na harufu murua ya nyama pori choma zilizokuwa zikigeuzwa kwa ustadi na wapishi mahiri. Wageni wakipata fursa ya kuonja ladha ya nyama pori huku wakijifunza kuhusu umuhimu wa uhifadhi endelevu wa wanyamapori kama sehemu ya utalii wa ndani na urithi wa rasilimali za taifa.


Tamasha hilo limeendelea kuwa jukwaa muhimu la kuelimisha, kuburudisha, na kuhamasisha jamii kuenzi thamani ya rasilimali wanyamapori kupitia utalii utalii wa ndani.




No comments:

Post a Comment