NA MWANDISHI WETU
UONGOZI wa Chuo cha Ufundi Farahika
kinachoendesha mitaala yake chini usimamizi wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Stadi (VETA) kimetangaza kuanza kufundisha kozi mpya nane ikiwemo ya
Uhasibu.
Mkuu wa Chuo hicho kilichopo
Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam ndani ya Chuo Kikuu cha St John, Aliko
Mmongele amesema kozi ya Uhasibu inafundishwa chini ya usimamizi wa Bodi ya
Uhasibu Tanzania (TAA).
Mmongele amefafanua kuwa kozi
nyingine mpya ambazo zitafundishwa chuoni hapo kwa gharama nafuu ni Ufundi
Bomba (Pumbling), Mapishi (Catering), Masoko (Sellesmanship), Mtoa huduma kwa
wateja (Customer Care), Msoma Mita za Maji (Watermeter Reading) na Business
Oparator.
Amefafanua kuwa lengo la kuanzisha
kozi hizo mpya ni kuwafikia vijana wengi na kuendelea kuunga mkono juhudi za
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Zanzibar katika
jitihada za kuwainua vijana kupitia elimu ya amali inayosaidia kuliondoa kundi
hilo katika utegemezi.
“Hiki ni chuo kimekuwa kikiendesha
kozi mbalimbali kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na Serikali ya Zanzibar na sasa tumeanzisha kozi mpya zitakazofundishwa pamoja
na zile zinazotolewa kwa mpango wa elimu bure.
“Ni dhahiri zitawafikia vijana
wengi wenye uhitaji wa kupata mafunzo ya ufundi stadi kama ambavyo Rais Dkt
Samia Suluhu Hassan anavyosisitiza kuhusu mafunzo ya amali kuifikisha kwenye kundi
kubwa la vijana ili waweze kujitengenezea ajira baada ya kuhitimu.
“Hivyo tunawakaribisha vijana
wote wa kitanzania kutoka mikoa yote hapa nchini kuja kupata mafunzo haya
ambayo yanaendeshwa chini ya mtaala wa Veta kwa tafsiri ya haraka maana yake
uwezi kutenganisha Chuo cha Furahika na
Veta, waje kwa wingi na hata wakiwa watano tunaanza na nao zipo kozi za muda
mfupi na mrefu,” amasema.
.png)




No comments:
Post a Comment