NA MWANDISHI WETU
IDRISA Ngatiche ameapishwa rasmi kuiongoza Kata ya Kinondoni katika nafasi ya udiwani kwa muhula wa pili na kuahidi kuendelea kuwatumikia wananchi wake kwa uaminifu mkubwa kama ambavyo imefanyika kwa kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025.
Diwani huyo, katika kipindi cha miaka 2020 hadi 2025 amefanikiwa kujenga barabara za ndani na kujenga zahanati, kuwasaidia wanawake kwa mikopo ya asilimia 10 ambayo imekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa kata hiyo kupata huduma ya afya kwa haraka tofauti na awali.
“Nashukuru leo nimeapa kwa ajili ya kuendelea kuwatumikia wananchi kwa muhula mwingine baada ya kushinda kwa kishindo katika Uchaguzi Mkuu ambao umepita kwa nafasi ya udiwani, kikubwa ni kumuomba Mwenyezi Mungu aendelee kunipa uhai na afya njema ili niweze kutimiza majukumu yangu vema kwa wananchi wangu,” amesema.
Ngatiche amekura kiapo leo Desemba 5, 2025 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni pamoja na madiwani wengine ili kuwatumikia wananchi wao kwa nafasi ya udiwani kwa kipindi cha mwaka 2025 hadi 2030.
Baada ya kuapishwa madiwani hao kupitia kikao cha Baraza la Madiwani walimchagua kwa kishindo, Songoro Mnyonge kuwa Meya kwa kipindi cha pili.





No comments:
Post a Comment