MECIRA WATUA UBALOZI WA MAREKANI NA KENYA WANAHARAKATI VURUGU OKTOBA 29 WAREJESHWE TANZANIA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, December 17, 2025

MECIRA WATUA UBALOZI WA MAREKANI NA KENYA WANAHARAKATI VURUGU OKTOBA 29 WAREJESHWE TANZANIA


NA MWANDISHI WETU


KITUO Cha Wanahabari Watetezi wa Rasilimali na Taarifa (MECIRA) ituma barua katika Balozi za Marekani na kuomba wanaharakati  wanaoishi katika mataifa hayo ambao wamehamasisha vurugu Oktoba 29 mwaka huu  warejeshwe Tanzania ili hatua zicjukuliwe dhidi yao.

Mwenyekti wa taasisi hiyo, Habibu Mchange.amebainisha hayo leo Disemba 17, 2025 jijini Dar es Salaam na kubainisha kuwa anaamini nchi hizo zinaendeshwa kwa msingi ya demokrasia na kuheshimu utu wa mataifa mengine hivyo hataweza kuruhusu ardhi yao itumike na baadhi ya watu kuharibu amani ya  nchi nyingine.

"Pia tumewaomba mabalozi wao hapa nchini kuhakikisha wanafikisha taarifa sahihi zisizo za upande mmoja katika mataifa yao na kuwaeleza kinagaubaga kuwa Tanzania ni tulivu na inaheshimu misingi ya utu na demokrasia," amesema.

Mchange amesisitiza kuwa Tanzania ni taifa huru lenye misingi imara ya sheria, utawala bora, amani na mshikamano wa kijamii. Nchi imeendelea kudumisha heshima ya utawala wa sheria na maadili ya kidemokrasia, jambo linalochangia maendeleo endelevu na utulivu wa jamii.

Ameongeza kuwa jitihada zozote za kuhamasisha wananchi zinapaswa kufanyika kwa uwazi, uadilifu na kwa kushirikiana na mamlaka halali za nchi, huku zikiheshimu misingi ya kisheria na maadili ya kidiplomasia. 

Amesema hali hiyo itasaidia kuepuka sintofahamu au athari zisizotarajiwa zinazoweza kuathiri amani na mshikamano wa taifa.

Pia  amesisitiza kuwa vyombo vya habari, wanahabari na watumiaji wa mitandao ya kijamii wanapaswa kuhakikisha taarifa zinazotolewa ni sahihi, zenye mizani na zinazoelezea muktadha wa kijamii na kisiasa. 


Mchange amefafanua kuwa hiyo itachangia uelewano na mshikamano wa kitaifa, badala ya kuunda mgawanyiko au kuchochea sintofahamu.

Aidha amewatahadharisha mataifa na wadau wa kimataifa kuendeleza diplomasia ya heshima, kushirikiana na mamlaka ya Tanzania, na kuepuka vitendo vinavyoweza kuonekana kama kuingilia masuala ya ndani ya nchi.


Ameongeza kuwa Ushirikiano wa kikanda na mazungumzo ya kidiplomasia ni msingi muhimu wa kudumisha amani, mshikamano na maendeleo ya wananchi.


No comments:

Post a Comment