ALIYEPATA KIGUGUMUZI WAKATI WA KUOMBA KURA KWA LUGHA YA KINGEREZA ASHINDA KUWAKILISHA BUNGE - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, February 6, 2026

ALIYEPATA KIGUGUMUZI WAKATI WA KUOMBA KURA KWA LUGHA YA KINGEREZA ASHINDA KUWAKILISHA BUNGE


Mbunge wa Jimbo la Ukonga (ACT) Bakari Shingo ambaye mapema leo Bungeni alipata kigugumizi wakati wa kujinadi kwa kutumia lugha ya Kingereza akiomba kura za Wabunge ili akaiwakilishe Nchi ya Tanzania katika Jukwaa la Maziwa Makuu akiwakilisha upande wa walio wachache Bungeni ameshinda nafasi hiyo kwa kura 242 kati ya wapiga kura 301.


Akitangaza matokeo hayo Katibu wa Bunge Baraka Leonard amewataja washindi katika uwakilisha wa Umoja wa Mabunge ya Nchi za Maziwa Makuu ambao ni Sylvia Sigula, Said Salim Hamad, Eng. Ezra Chiwelesa Cosmas Bulala na Bakari Shingo.

"Nilivyoitwa na Spika, wakati nainuka kidole kikagusa keypad (kitufe) kwahiyo ikawa imepunguza sauti, ikawa imeniondoa kwenye reli na unajua Bunge ni suala la uzoefu. Sasa katika kuitafuta ikawa pia imenishinda kuirudisha unajua mambo ya teknolojia.

-

Lugha inaweza ikawa ni tatizo kwa Sababu mimi  sio lugha yangu ya asili na sio suala la ajabu na sio issues sana kama wengine wanavyosema, tuchukulie watu wameamua kujadili na sio mbaya watu kujadili kwa namna watu wanavyoona kwanza lugha ya kingereza sio kipaumbele changu sana, nimesoma" Amesema mbunge wa Jimbo la Ukonga Bakari Shingo.

Credit - Paza Sauti

No comments:

Post a Comment