GWIJI wa muziki wa Taarab hapa Tanzania , Ally Hemed 'Ally Star', anatarajiwa kuzikwa kesho Feb, 4, 2026 Kilosa mkoani Morogoro.
Taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa bendi ya Tanzania One Theater TOT, Khadija Kopa, amesema mchakato wa safari ya kwenda Kilosa inatarajiwa kuanza kesho saa 2:00 asubuhi.
Amefafanua kuwa waombolezaji watakutana katika eneo la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuanzia saa 1:00 asubuhi kabla ya kuanza safari.
Mkurugenzi huyo, amesema kwamba mazishi ya nguli huyo ambaye alikuwa mtunzi mahiri wa nyimbo za maadhi ya taarab hapa nchini yatafanyika mara baada ya msafara kuwasili Kilosa.
Ally Star alifariki dunia leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.
Nyota huyo enzo za uhai wake, alijizolea umaarufu kupitia nyimbo za mahadhi ya Pwani, zikiwemo Zumbukuku, Natanga na Njia.
.png)




No comments:
Post a Comment