MAFYA BOXING PROMOTION YAMLILIA BONDIA CHOKUDUSO, KUZIKWA LEO DAR - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, February 10, 2026

MAFYA BOXING PROMOTION YAMLILIA BONDIA CHOKUDUSO, KUZIKWA LEO DAR

 


NA MWANDISHI WETU 

UONGOZI wa Mafya Boxing chini ya Mkurugenzi wake Ally Zayumba wametoa pole kwa familia ya masumbwi nchini kutokana na kifo cha bondia mkongwe maarufu 'Chokiduso'

Taarifa za kifo cha mkongwe huyo wa ngumi nchini zisikika leo na msiba upo Manzese na atazikwa leo Februari 10, 2026 jijini Dar es Salaam katika Makaburi ya Mianzini Mburahati.

Zayumba wakati alitambulisha pambano litakalofanyika Februari 15 mwaka huu, 'Sparring Game' ikiwa ni mchakato wa kuelekea  msimu wa nane wa 'Knockout ya Mama', April 25 mwaka huu, alisema wamesikitishwa na msiba huo mzito wa chakuduso

"Tunamuomba ampumzishe chakudoso mahali pema na kumuondolea adhabu ya kaburi," amesema.

Chokuduso enzi za uhai wake aliwahi kuwa Kocha na mchezaji wa zamani wa ngumi wa klabu ya ngumi Urafiki.

No comments:

Post a Comment