NA MWANDISHI WETU
Waandishi wa habari Nchini wameaswa kutoa taarifa sahihi kwa Jamii kihusu Lishe.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Lishe Nchini TFNC Dkt. Germana Leyna,wakati Akizungumza leo kwenye Semina ya Waandishi wa habari, yenye lengo la kuwajengea uwezo wanahabari kuhusu Lishe.
Aidha,Dkt Leyna, amesema kumekuwa na taarifa mbalimbali kwenye jamii zenye lengo la kupotosha kuhusu suala zima la lishe, jambo linaloisababishia jamii kukosa elimu na taarifa sahihi kuhusu Lishe.
Amesema kuwa Jamii bado inakabiliwa na Changamoto ya suala zoma la Lishe, jambo linalochangia ongezeko la magonjwa mengi yasiyo ya kuambikiza yayosababishwa na ulaji mbaya wa Chakula.
Katika hatua nyingine Dkt. Leyna amesema kuwa Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Chakula na Lishe umeeleza Changamoto ya Lishe bado ni kubwa, ikiwa ni pamoja na Udumavu kwa asilimia 30 kwa Watoto wenye umri wa miaka 5. Amesema Mikoa ya Njombe, Iringa na Rukwa inaongoza kwa kua na kiwango kikubwa cha Udumavu.
Semina hiyo imelenga kuwajengea waandishi wa habari uelewa mpana kuhusu umuhimu wa kuelimisha jamii juu ya ulaji wa mlo kamili na wenye lishe bora, ili kusaidia kupunguza changamoto za utapiamlo na magonjwa yatokanayo na lishe duni.
Taasisi ya Lishe na Chakula Tanzania ilisisitiza kuwa ushirikiano kati ya wadau wa afya, vyombo vya habari na jamii kwa ujumla ni nguzo muhimu katika kujenga taifa lenye afya bora na nguvu kazi imara.





No comments:
Post a Comment