TRA PWANI ULIPAJI KODI BANDARI YA BAGAMOYO KUWA RAFIKI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, February 28, 2026

TRA PWANI ULIPAJI KODI BANDARI YA BAGAMOYO KUWA RAFIKI


NA MWANDISHI, WETU BAGAMOYO.


MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa Pwani imewatoa hofu  wafanyabiashara wa mafuta ya kula kwenye Bandari ya Bagamoyo kuwa kodi itakuwa rafiki.


Akizungumza na wafanyabiashara wa mafuta ya kula kwenye Bandari hiyo Meneja wa TRA Mkoa huo Masawa Masawa amesema kuwa changamoto iliyopo ni malalamiko ya wafanyabiashara kulalamikia bei ya kodi ya mafuta yanayotoka Zanzibar.


Masawa amesema kuwa changamoto hiyo ambayo ilianza tangu Desemba mwaka jana ilisababisha wafanyabiashara hao kutofanya biashara wakidai kodi ni kubwa.


"Chagamoto hiyo tumeipokea na kuna timu iliundwa ili kufuatilia na itatoa majibu tarehe Mosi Machi kwa kuwa na utaratibu mwingine hivyo wafanyabiashara hao wanapaswa kuwa na subira katika kipindi hicho,"amesema Masawa.


Meneja Msaidizi wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa Mkoa wa Pwani Melinda Matinyi amesema kuwa wafanyabiashara hao ni muhimu kwani wanachangia mapato ya serikali kwani ulipaji kodi ni muhimu.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Shaibu Ndemanga alisema kuwa wananchi wengi wanategemea biashara ya mafuta na kuna wadau wengi wanategemea shughuli zinazohusiana na biashara ya mafuta.


Naye Diwani wa Kata ya Dunda Amiry Mpwimbwi amesema kuwa eneo hilo la Bandari linatoa ajira zaidi ya 8,000 hivyo kutokana na shughuli kutofanyika kumesababisha serikali kukosa mapato.


Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa Mafuta kwenye Bandari hiyo Shaban Hamsini amesema kuwa hali imeshakuwa mbaya kwani wanategemea shughuli hizo kuendeshea maisha yao.



No comments:

Post a Comment