Watumishi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) walioshiriki kikao cha pili cha Baraza la Wafanyakazi jijini Mwanza Machi 7, 2026 wametembelea Hifadhi ya Kisiwa cha Saanane.
Ziara ya watumishi wa BRELA kutembelea Hifadhi hiyo imelenga kuhamasisha utalii wa ndani na imefanyika baada ya kumalizika kwa kikao cha pili cha Baraza la Wafanyakazi wa BRELA kilichoketi jijiji humo kujadili ajenda nane za kiutendaji na za kimkakati.
Aidha, katika kikao hicho cha Baraza la Wafanyakazi wa BRELA watumishi walipata fursa ya kupatiwa mafunzo juu ya Afya ya Akili kutoka kwa mtaalamu wa saikolojia na magonjwa ya akili Dkt. Swai Japhet wakati elimu ya fedha na uwekezaji ilitolewa na CPA (T) Emilian Busara.
Ikumbukwe kuwa kikao cha pili cha Baraza la Wafanyakazi wa BRELA kilifunguliwa rasmi na Waziri wa Viwanda na Biashara Judith Kapinga tarehe 04 Machi 2026 akisisitiza umuhimu wa taasisi kutumia mifumo ya kidigitali iliyoboreshwa ili kumuwezesha mfanyabiasha kufanya biashara kwa urahisi.
Kikao hicho cha siku mbili kilifanyika kuanzia tarehe 04 hadi 05 Machi 2026, kilifungwa na Mwenyekiti wake ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Godfrey Nyaisa baada ya washiriki kuridhia na kupitisha ajenda za kiutendaji na za kimkakati zilizojadiliwa kwa siku zote mbili.
![]() |







No comments:
Post a Comment