Waombolezaji wakishusha kaburini jeneza lenye mwili wa Gabriel Ambakisye Mwaibale wakati wa mazishi yake yaliyofanyika Makaburi ya City Yombo Dovya Temeke Jijini Dar es Salaam Julai 16, 2026.
............................................
Wanadamu
tumetakiwa kuishi maisha ya kumjua Mungu kwani hapa duniani ni wageni tunapita.
Ombi hilo
limetolewa na Mchungaji Michael Ndimbwa wa Kanisa la Pentekoste Tanzania (KLPT)
Tandika Jijini Dar es Salaam wakati akiongoza ibada ya mazishi ya Gabriel
Mwaibale iliyofanyika Julai 16, 2026 Yombo Dovya Njia Panda ya kwa Mwinyi.
Alisema
msiba wowote unaleta huzuni kwa kuondokewa na mpendwa wao.
“Maisha ya aliyefariki yana maana kwa wale wanaoguswa naye na kama hayana mguso yanakuwa hayana maana,’ alisema Ndimbwa.
Alisema hapa
duniani sisi wote ni wageni hivyo tunapaswa kujua maisha yetu si kitu chochote
mbele ya Mwenyezi Mungu.
Ndimbwa
alisema kila mtu anapaswa kuishi maisha yenye maana ya kumjua Mungu badala ya
kutegemea mambo ya duniani.
Akitolea
mfano wa tajiri mmoja ambaye alilazimika kuuza mali na gari lake la kifahari baada ya
kupata ugonjwa wa moyo ili atafute maisha yenye maana.
Alisema
changamoto kubwa tuliyonayo ni kushindwa kujitambua kwani mwanadamu aliyezaliwa
na mwanamke siku zake siyo nyingi hivyo kila mmoja wetu anapaswa kujiuliza kama
anaishi maisha ya maana.
Alisema
maisha ya kumjua Mungu yana changamoto kubwa mbele ya dunia lakini mbele ya
Mungu yatamfanya mtu anaye muamini kuwa salama.
“Kila mtu atafakari safari ya maisha yake hapa duniani na uamuzi wa kufanya kati ya kutafuta maisha yasiyo na maana au yenye maana,” alisema Mchnguaji Ndimbwa.
Diwani wa
Kata ya Makangarawe wilayani Temeke, Fadhil Mboga, akitoa salamu za rambirambi
wakati wa ibada hiyo aliwashukuru viongozi mbalimbali, wakiwepo wa dini zaidi
ya 10 na wananchi walioshiriki kwenye msiba huo na kusisitiza ushirikiano huo
uzidi kuendelea.
Mazishi ya
Gabriel Ambakisye Mwaibale ambaye alifariki Julai 14, 2026 Hosptali ya Rufaa ya
Temeke alikokuwa akitibiwa kutokana na maradhi ya figo yalifanyika Julai 16,
2026 katika Makaburi ya City Yombo Dovya.
Mchungaji Michael Ndimbwa wa Kanisa la Pentekoste Tanzania (KLPT) Tandika Jijini Dar es Salaam, akiongoza ibada ya mazishi ya Gabriel Mwaibale.
Baba wa Gabriel Mwaibale akiwa ameshika tama wakati wa ibada hiyo.
Mama Mzazi wa Gabriel Mwaibale akilia kwa uchungu.
Jirani wa Wazazi wa marehemu, Mzee Alexander Mwakalasya akiwajibika ipasavyo wakati wa msiba huo.
Mchungaji Justine Kiwovewe (kushoto) na Mchungaji Michael Ndimbwa wa Kanisa la
KLPT wakiombea jeneza lenye mwili wa Gabriel wakati wa ibada hiyo.
Marehemu Gabriel Mwaibale enzi za uhai wake.
Waombolezaji, ndugu, jamaa, marafiki na majirani wakiwa kwenye ibada hiyo.
Kaka wa marehemu Kulwa Mwaibale akimfariji mama mkubwa wa Gabriel wakati wa uagaji wa mwili.
Habari hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale simu namba 0754362990.





No comments:
Post a Comment