CHALAMILA AWAONGOZA WANAWAKE MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI DAR - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, March 8, 2026

CHALAMILA AWAONGOZA WANAWAKE MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI DAR


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameongoza wanawake wa Mkoa huo katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake Kimkoa yaliyofanyika kwenye viwanja vya barafu Mburahati Wilaya ya Ubungo.


 Kipitia maadhimisho hayo amemkabidhi Mama wa Marehemu Steven Kanumba "Mama Kanumba" Gari mpya aina Harier  iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan


Akizungumza katika maadhimisho hayo  Chalamila pamoja na kumpongeza Rais Dkt Samia ambaye ni mwanamke alieweza kuiongoza Tanzania kwa mafanikio makubwa ambapo amesema maadhimisho haya yanatoa fursa ya uwepo wa usawa wa kijinsia na kuepuka vitendo vya ukatili kwa wanawake na wasichana huku akiwataka wasanii, wanawake na wanaume kuwakumbuka mama zao wanapopata mafanikio


Amesema akima mama wengi wanaishi kwenye mazingira magumu huko vijijini ambapo amesema ni muhimu kwa watoto kutambua kuwa mama zao walitaabika kuwazaa na kuwalea hivyo ni muhimu kuwathamini huku amkimzungumzia Mama Kanumba ambae kwa mapenzi ya Mungu mwanae Steven Kanumba alifariki dunia wakati ndio ameanza kupata mafanikio hivyo Rais Samia amempa gari hilo kumfariji baada kuona kupitia vyombo vya habari akiomba kupatiwa usafiri


Aidha, Chalamila ametaja miongoni mwa changamoto zinazowakabili wanawake ikiwemo magonjwa ya saratani ya shingo ya kizazi na matiti, uwepo wa vitendo vya ukatili ikwemo vipigo ambapo amewataka wanawake kujiwekea mipamgo madhubuti ya kujiimarisha kiuchumi ili kuepuka vitendo vya ukatili na amewataka kujiepusha na mikopo isiyokuwa na malengo


Kwa upande waMbunge wa Jimbo la Ubungo na Waziri wa Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amewaahidi wanawake kuwa dira zote za maendeleo zinazoandaliwa na serikali zitakua jumuishi ili kuhalikisha wanawake wanakua ni sehemu ua wanufaika bila kuachwa myuma


Sanjari na hilo Makamu Mwenyekiti wa jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi Hidaya Njaidi amewataka wanawake kuendelea kijiunga kwenye vikumdi na kufanya kazi kwa vikundi ili kunufaika na fursa mbalimbali za uwezeshwaji huku akiomba uwepo wa magulio chini ya jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi ili wanawake wapate masoko


Maadhimisho ya siku ya wanawake hufanyika duniani kote machi nane ya kila mwaka ambapo kwa Mkoa wa Dar es Salaam yamefanyika katika viwanja vya barafu mburahati Wilayani Ubungo na yamebeba kaulimbiu isemayo "Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana ni Msingi Jumuishi kufikia Dira ya Maendeleo ya Mwaka 2050"





No comments:

Post a Comment