NAIBU WAZIRI WA NISHATI AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI WA GO PLANT TANZANIA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, March 3, 2026

NAIBU WAZIRI WA NISHATI AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI WA GO PLANT TANZANIA



NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba amekutana na Mkurugenzi wa Go Plant Tanzania, Emmanuel Likida kwa lengo la kujadili namna ya kushirikiana katika maandalizi ya Mjadala (Debate) wa Clean Cooking Solutions utakaowahusisha wanafunzi wa shule za Sekondari katika Halmashauri za Mkoa wa Dodoma. 


Katika kikao hicho, pande zote mbili zimejadili umuhimu wa kuwajengea vijana uelewa wa mapema kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia, athari za matumizi ya nishati zisizo safi kwa afya na mazingira, pamoja na fursa zilizopo katika ubunifu na ujasiriamali wa suluhisho za upishi safi.



Mjadala huo unatarajiwa kuwa jukwaa la kielimu na kimkakati la kukuza uelewa, kuchochea fikra bunifu, na kuibua mabalozi vijana wa Nishati Safi katika jamii.


Kikao hicho kimefanyika leo Machi 03,2026 katika Ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo Mtumba, jijini Dodoma.



No comments:

Post a Comment