NA MWANDISHI WETU
MWENYEKITI wa Tume huru ya kuchunguza matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29,2025, Jaji Mstaafu Othman Chande amesisitiza kuwa Tume hiyo inajitegemea kwa kila kitu.
Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo Jumatano Aprili 08, 2026, Jaji mstaafu Chande amesisitiza kwa sasa Time hiyo ipo katika hatua za mwisho kukamilisha kazi waliyopewa kwa kuchambua ushahidi kwa kina ili kuhakikisha ripoti yao inakuwa na ubora unaotakiwa na itatolewa kwa lugha ya Kiswahili na kutafsiriwa kwa lugha ya Kiingereza.
"Tume inajitegemea kwa kila kitu, Tume ndio mhariri, ndio msahihishaji na mamlaka iliyotupa kazi tunaonana nayo wakati tunapewa hadidu za rejea na wakati tunamkabidhi ripoti ya mwisho. Hakuna mtu yoyote hapa katikati, hatuna dalali, tunafanya kazi yetu tumalizie na tupo katika hatua ya mwisho katika kutafsiri." Amesema Jaji mstaafu Chande.
Tume hiyo kwa sasa inatarajiwa kukabidhi ripoti yake kabla au April 24, 2026 baada ya hivi karibuni kuongezewa mud ana Mamlaka iliyoipa kazi hiyo Tume hiyo ya Uchunguzi.





No comments:
Post a Comment