NA MWANDISHI WETU
WITO Umetolewa kwa Watanzania kujitokeza kuchangia ujenzi jengo jipya la Hospitali ya Moyo ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC).
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na Waandishi wa Habari, Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Prof. Gileard Masenga amebainisha kwamba gharama ujenzi huo unagharimu Shilingi Billioni 25 na vifaa tiba vya Billioni 25.
"Hospitali hii itakuwa ya ghorofa tatu, itakayojumuisha vyumba viwili vya upasuaji wa moyo, maabara mbili za uchunguzi wa mishipa ya moyo, vyumba vya wagonjwa mahututi, vitengo vya uangalizi maalum baada ya ICU, vitanda 102 vya wagonjwa wa ndani, kliniki za wagonjwa wa nje, kitengo cha urekenishaji wa afya ya moyo na maabara za uchunguzi wa huduma za dawa,"amesema.
Amefafanua kwamba KCMC tayari imeingia mabakuliano ya ushirikiano na wadau wa kimataifa ambao wamekubali kufadhili ujenzi huo kwa asilimia 90 ya ujenzi huo na iliyobaki ni kwa watanzania kuchangia ili kufanikisha ujenzi huo unaotarajiwa kukamilika Julai mwakani.
Prof Masenga amesema kwamba namba za kutuma mchango huo ni Bank of Africa - 04563580007, CRDB - 0150686858800, NMB - 40310194610 na NBC 017172000770
Pia kupitia mitandao ya simu za mkononi ni Mix by Yas - 15175376 na Halotel - 23758475.
"Kupitia vyombo vya habari, tunatoa wito wa dhati kwa watanzania wote popote walipo ndani na nje ya nchi kuungana katika juhudi hii ya kitaifa na mradi huu ni wa kulinda maisha ya ndugu zetu, wazazi wetu, watoto wetu na vizazi vijavyo," amesisitiza.
Pia amesema kwa wale wanaopenda kutoa michango yao ana kwa ana wanakaribishwa kufika Hospital ya KCMC mkoani Kilimanjaro.








No comments:
Post a Comment