NA MWANDISHI.WETU
WATUMISHI wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) leo Mei 23, 2026 wameshiriki Viwango Marathon 2026 iliyofanyika katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Maadhimisho hayo yanaakisi mafanikio makubwa ya shirika hilo katika kusimamia ubora na usalama wa bidhaa pamoja na huduma mbalimbali nchini. Mbio hizo zilihusisha kilomita 21, kilomita 10, kilomita 5 na kilomita 2 huku zikilenga kuhamasisha afya na kuimarisha utimamu wa mwili kwa washiriki.
BRELA imeshiriki Viwango Marathon kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi mbalimbali, kuthamini mchango wa wadau wake, na kukuza mshikamano katika utendaji kazi. Ushiriki huo pia umeonesha dhamira ya BRELA katika kuendeleza mahusiano bora ya kikazi na taasisi nyingine pamoja na kuimarisha afya na utimamu wa mwili kwa watumishi wake.






No comments:
Post a Comment