CHUO CHA UDEREVA FUTURE WORLD KUTOA ELIMU USALAMA BARABARANI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, May 27, 2026

CHUO CHA UDEREVA FUTURE WORLD KUTOA ELIMU USALAMA BARABARANI


NA MWANDISHI WETU 


CHUO Cha  udereva Cha Future World kilichopo Chanika Ilala jijini Dar es Salaam  kimeendelea kuwaonoa madereva wa magari ya abiria na mizigo huku kikisitiza kuwa mkakati wake ni kutoa mafunzo ya elimu ya usalama barabarani kwa lengo la kumaliza jinamizi za ajali za barabarani nchini.


Kwa mujibu wa mkurugenzi Mtendaji na mmiliki wa Chuo hicho Robert Mkolla ametaja sababu tatu kuu ambazo ndizo zimekuwa chanzo cha qjali za barabarani na ili kuondoa sababu hizo  ni lazima  dereva kupatiwa elimu na ndio maana chuo chake kimekuwa mstari wa mbele kutoa elimu kwa Madereva Nchini.


Akizungumza  Mei 26,2026 wakati wa kupokea madereva waliojiunga na chuo hicho,madereva waliomaliza masomo yao kwa kufanya mihatihani pamoja na kutambulisha kozi mpya ya  mafunzo maalum kwa wakufunzi wa udereva kutoka vyuo mbalimbali nchini  mkurugenzi Mkolla ametumia nafasi kueleza kwamba  ajali za barabarani nyingi  tafiti zinaonesha zinatokana na makosa ya kibinadamu na hasa makosa ya dereva.


“Sababu tatu ambazo zimekuwa zikisababisha ajali za barabarani zinatokana na uzembe, upuuzaji na kutokujua.Hakuna binadamu mwenye akili timamu asiyejua madhara ya ajali ,kinachosababisha ajali  ni kutojua ,kupuuza au kuzembea 


         WANAFUNZI 


Wanafunzi Erasto John na George Steven Wamesema baada ya Serikali kuona hatari zilipo mbele katika matumizi ya Barabara  kupitia vyombo husika kimekuwa na madhara makubwa na kupeleka upotevu wa maisha ya watu wengi na kusababisha  uhalibifu sa miundombinu na kupelekea uwepo wa wategemezi hayo yote yanayokana na kukosa elimu .


Wamesema kutokana  na hali hiyo ndio wamelazimika kuja kwenye chuo hicho ili kupata elimu ya usalama ya Barabara na hasa katika udereva wa kujihami ambapo udereva huo ndio unaepusha uwepo wa ajali zote za Barabarani.


Wameongeza kuwa kabla ya kwenda kusoma walikuwa wanaendesha gari kwa kutokujua kwani mtu akipata leseni  kwa njia zake basi ameona amemaliza sasa kutokana na msukumo wa Serikali wameona Kuna ulazima wa kuingia darasani . 


          WAKUFUNZI 


Kwaupande wao wakufunzi Egnas Bethod na Elbariki Juma walimu kutoka vyuo tofauti hapa nchini wamesema  lengo la kuja chuo hicho Cha future world  ni kupata kozi ya ukufunzi  na kwamba Kuna mabadiliko mengi yamekuwa yakitokea katika tasinia ya udereva .


Wamesema hivi sasa wakipiga hesabu kuazia mwaka Jana hadi sasa mfumo umekuwa ukibadilika karibu mara tatu hadi nne  ambapo huko nyuma ilikuwa rahisi kupata Leseni  ambapo ilikuwa mtu anafanya mafunzo siku mbili au hajafanya kabisa lakini anapata leseni kwa njia zake lakini ikabadilika tena ,sasa mtu ni lazima aingie darasani apate cheti ndio apate leseni na sasa kwenye vyuo pia  mambo yamebadilika na ndio maana wamelazimika nawao kwenda kuongeza maarifa.


Wameongeza hivi sasa ili chuo kiwe na hadhi ya kutoa cheti kwa wanafunzi lazima wakufunzi na wenyewe wawe na vigenzo ambavyo usajili wake umetoka Jeshi la Polisi  hivyo imewalazimu nao kurudi darani ili vyuo vyao viweze kuwa na sifa ya kutoa vyeti na wanafunzi kupata Leseni.







No comments:

Post a Comment