DKT MSUYA AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUWAKEMEA WANASIASA WANAOPANDIKIZA CHUKI KWA WATANZANIA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, May 22, 2026

DKT MSUYA AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUWAKEMEA WANASIASA WANAOPANDIKIZA CHUKI KWA WATANZANIA


NA MWANDISHI WETU

WITO umetolewa kwa viongozi wa dini nchini kuwakemea baadhi ya wanasiasa wanaotumia lugha zisizo za stara majukwaani kuacha kufanya hivyo ili kulinda amani ya nchi.

Mdau wa masuala ya siasa hapa nchini Dkt David Msuya ametoa wito huo leo wakati akizungumzia na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam na kusisitiza amani ya nchi ikipotea ni vigumu kuirejesha.

"Nawaomba sana viongozi wetu wa dini kuilinda amani yetu kwa kuhakikisha wanawakemea wanasiasa wanaotoa maneno ya uchochezi na kukumbusha yaliyotokea Oktoba  29 mwaka jana.

Tume ilishatoa maoni yake na yanaendelea kufanyiwa kazi na Rais wetu, ili kuhakikisha haki inatendeka na nchi inakuwa salama, sasa hawa baadhi wanaopanda majukwaani na  kuanza kukumbusha yalitokea Oktoba 29 ni vema viongozi wa dini wakawakemea kwa kuwa hilo suala linaendelea kufanyiwa kazi.


Bado watu wanamachungu ya yale yaliyotokea hivyo wanakiwa kuendelea kupewa faraja ili kuweka utulivu katika mioyo yao na si kuendelea kuwapa maumivu na kuwapandikiza chuki, sasa wanapotokea wengine kuanza kuwakupa majungu, hiyo si sawa na kuwa kuwa Mimi ni Mtanzania hilo siwezi kulifumbia macho,' amesema Dkt.

Amesema baadhi ya kauli kutoka kwa viongozi wa kisiasa zimekuwa zikiumiza mioyo ya Watanzania badala ya kuleta maridhiano na mshikamano wa kitaifa.


Ameeleza kuwa Tanzania ni nchi ya Watanzania wote, hivyo hakuna sababu ya kutumia siasa kuleta migawanyiko wakati wananchi wanahitaji kuona maendeleo ya haraka katika sekta mbalimbali ikiwemo barabara, afya, elimu na uwekezaji. Alisisitiza kuwa wananchi wanataka kuona miradi ikikamilika kwa wakati na fedha za maendeleo zikitumika kwa uadilifu.


Dk Msuya alisema viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kuendelea kuiombea nchi amani pamoja na kuwashauri viongozi wa kisiasa kuzungumza kwa hekima wanapokutana na wananchi katika mikutano yao ya kisiasa. Aliongeza kuwa maneno ya hasira na mihemko yanaweza kuchochea vurugu na kuathiri mshikamano wa taifa.


Aidha, alisema wawekezaji hawawezi kuwekeza katika mazingira yenye migogoro na vurugu, hivyo Watanzania wanapaswa kuhubiri amani ili kuvutia uwekezaji na kuongeza ajira kwa vijana. Alitolea mfano wa miradi na viwanda vinavyoendelea kujengwa nchini kuwa ni miongoni mwa maendeleo ambayo wananchi wanapaswa kuyapa kipaumbele.


Katika hatua nyingine, Dk Msuya aliitaka serikali kuendelea kusikiliza maoni ya wananchi na kuchukua hatua pale panapobidi marekebisho kufanyika, akisisitiza kuwa kukosolewa si jambo baya bali ni njia ya kujirekebisha na kuboresha utendaji kwa maslahi ya taifa.


Pia alikumbusha kuwa misingi ya amani, upendo na mshikamano iliyowekwa na Julius Nyerere inapaswa kuendelea kuheshimiwa, huku Watanzania wakitakiwa kutanguliza utaifa mbele.


Ameongeza kuwa wanasiasa wanachotakiwa kupigia kelele kwa sasa ni kuhusu miradi ya maendeleo ambayo inasuasua kukamilika kwa wakati na si kuumiza miyo ya watu na kuwapandikiza chuki zinazoweza kuliingiza taifa katika hali mbaya.

                 

No comments:

Post a Comment