WAJASIRIMALI STENDI YA MAGUFULI WAKUBALI KUREJEA KWENYE VIBANDA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, May 10, 2026

WAJASIRIMALI STENDI YA MAGUFULI WAKUBALI KUREJEA KWENYE VIBANDA


 NA MWANDISHI WETU 

WAJASIRIAMALI wadogo wa Stendi ya Magufuli wamekubali kurejea kwenye vizimba walivyopangiwa na uongozi wa stendi.


John Shayo mmoja wa wafanyabiashara waliorejea kwenye vizimba  kwa niaba ya wenzake amesema kwamba wamekubali  maelekeo waliopewa na uongozi wa stendi hiyo


"Sisi kama 2afanyabiashara wadogo tuliokuwa tumeweka biashara zetu ndani ya stendi tumekubali maelekezo yaliyotolewa na uongozi kwamba turudi kwenye vizimba Kisha huku tuje kwa ajili ya kufanya biashara za kubeba mikononi tu ",amesema


Naye Mwenyekiti wa Jengo la Abiria,  Haruna Silanda amesema kurejea kwa wafanyabiashara wadogo kutaleta usawa na mivutano isiyo na tija ,hivyo anawashukuru kundi hilo kukubali maelekezo yaliyotolewa na uongozi wa stendi na ni dhahiri umoja na mshikamano umerejea.


"Kwetu kama viongozi tumepata faraja kuona wenzetu kukubali kurejea kwenye vizimba na hii itasaidia wao kulipa kodi itakayosaidia kuongeza mapato ya stend,i" amesema


Kwa upande wa mjumbe wa jengo la abiria Rebeca Bigawa ameiomba serikali kurudisha mabasi ya abiria yanayoanzia sehemu nyingune yarudi stendi kuu ya mabasi ili abria waweze kuongezeka na wafanyabiashara hao waweze kupata wateja kama ilivyokuwa hapo awali.


"Kwa kwelinbiashara kwa sasa ni ngumu kutokana na baadhi ya mabasi kuanzia safari  zao nje ya stendi kuu na kupelekea kukosana kwa abiria wengi ndani ya stendi, Ombi letu tunamuomba  Rais wetu atuangalie kwa jicho la huruma ili mabasi yote yaanzia safari zake hapa",amesema


Awali ,Meneja wa stendi hiyo,Isaac Kasebo amesema waliweka utaratibu wa ambao walikuwa wakiusimamia wa kupanga wafanyabiashara kukaa kwa utaratibu katika maeneo ya kituo yanayotambulika kisheria.


Alisema katika kutekeleza mpango huo walianza na wafanyabishara ambao walikuwa wanapanga biashara zao katika eneo la kushusha na kupakia abiri ambapo kimsingi walijuwa wanafanya makosa.


Aliongeza kuwa kabla ya kuwaondoa walitoa elimu kufuatia na tangazo muda na sehemu wanayotakiwa kwenda kupata vibanda vyao.


"Na juzi Mei 5, 2026 mchakato huo wa kuwaondoa na kuwapatia vibanda na jambo hilo limekamilika kwa asilimia 100," amesema.

No comments:

Post a Comment