WAPIGA DEBE STENDI YA MABASI MAGUFULI KUFUKUZWA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, May 10, 2026

WAPIGA DEBE STENDI YA MABASI MAGUFULI KUFUKUZWA


 NA MWANDISHI WETU 


WAPIGA debe katika Kituo Kikuu Cha Mabasi Cha Magufuli wametakiwa kuondoka kabla ya kuondolewa siku chache zijazo.


Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake, mwishoni mwa wiki iliyopita, Meneja wa standi hiyo, Isaac Kasebo, amesema kwamba hawawajitaji wapiga debe hao ambao hawapo kisheria.


"Tayari tumeanza mazungumzo na wamiliki wa mabasi kuhamikisha hawawatumia wapiga debe hao ambao wamekuwa kero kwa abiria.


Pia wakati mazungumzo yanaendelea kati yetu na wamiliki wa mabasi ni vema, wapiga debe ambao wako ndani ya mipaka ya standi yetu wakatafuta shughuli nyingine au wakajisajili kwa viongozi wa mabasi ili watambulike tofauti na hivyo siku za kuwaondoa zinahesabika," amesema.

No comments:

Post a Comment