DKT. NCHIMBI ATEMBELEA BANDA LA TANESCO - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, June 5, 2026

DKT. NCHIMBI ATEMBELEA BANDA LA TANESCO


MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ametembelea banda la  Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) kwenye kilele cha Maonesho ya Siku ya Mazingira Duniani  yanayofanyika jijini Dodoma. 


Balozi Dkt. Nchimbi ametembelea banda la  hilo leo Juni 5, 2026 ambapo amepata nafasi  ya kuelezwa miradi mbalimbali inayotekelezwa na shirika hilo  ikiwemo matumizi ya Nishati Safi ya kupikia  kwa umeme pamoja na utunzaji wa mazingira kwenye vyanzo vya uzalishaji wa umeme.


Akitoa  maelezo kwa Balozi Dkt.Nchimbi Mkuu wa Kitengo  cha Mazingira Wizara ya Nishati Emmilian Nyanda ameeleza  kuwa TANESCO imekuwa ikifanya jitihada kubwa za kutoa elimu ya umuhimu wa Nishati Safi ya kupikia kwa Umeme kwa lengo la kuhakikisha kila mwananchi anashiriki  kwenye suala la utunzaji wa Mazingira.


Maonesho ya mwaka ya mazingira 2026 yalikuwa na kauli mbiu isemayo  Dira 2050, Tuwajibike Kukijanisha Tanzania.

No comments:

Post a Comment