TANZANIA KUENDELEA KUIMARISHA UKUAJI WA MIJI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, July 22, 2026

TANZANIA KUENDELEA KUIMARISHA UKUAJI WA MIJI

 


NA OWM- TAMISEMI, NEW YORK, MAREKANI 


SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kusimamia ukuaji wa miji nchini sambamba na kutenga fedha ili kuimarisha utoaji wa huduma za jamii,


Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Sospeter Mtwale  katika kikao cha 80 cha Umoja wa Mataifa kuhusu Mapitio ya New Urban Agenda kilichofanyika Julai 16-17, 2026 kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, Mjini New York, Marekani. 


Katika hotuba yake aliyoitoa wakati wa kikao hicho, Mtwale  amesema kuwa Serikali itaendelea kutenga fedha kuimarisha miji nchini, ikiwemo kushirikiana na wadau wengine kupata fedha za ujenzi miji ya kisasa na kuimarisha utoaji wa huduma za jamii.  


Katika Kikao hicho pia Bw. Mtwale alipata fursa ya kuzungumzia kuhusu hatua zinazochukuliwa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi,  majanga na uchafuzi wa mazingira kwenye miji ya Tanzania.


Ameelezea kuhusu jitihada zinazochukuliwa kuboresha miji ili isiathiriwe na mafuriko au majanga mengine, akitolea mfano uboreshaji wa Bonde la msimbazi kupitia mradi wa uendelezaji wa Jiji la Dar es Slaam(Dar es Salaam Metropolitan Development Project- DMDP).


Kwa upande wake Mkuregenzi wa Miundombinu kutoka OWM-TAMISEMI, Mhandisi Gilbert Mwoga ambaye pia ameshiriki katika kikao hicho amesema lengo la kikao hicho ni kufanya mapitio ya kuchochea kasi ya utekelezaji wa ujenzi wa miji endelevu, kujadili changamoto ya makazi bora mijini na ajenda ya miji mipya.


Katika kufikia lengo hilo  Mhandisi Mwoga amesema OWM-TAMISEMI imekuwa ikiboresha miundombinu ya barabara na majengo ya kutolea huduma kama vile masoko na na vituo vya mabasi katika maeneo ya mijini.


“Utekelezaji na uboreshaji wa miundombinu hii unafanyika kupitia mradi wa DMDP, TACTIC  na bajeti ya Serikali Kuu, katika  Manispaa nne  za mkoa wa Dar es Salaam na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na mradi wa TACTIC katika majiji matano,Manispaa 18 na miji 12,” amefafanua Mhandisi Mwoga,.


Mhandisi Mwoga ameeleza kuwa vigezo vinavyotumika katika uendelezaji wa miji  kinatokana nani idadi na kasi kubwa ua ongezeko la watu kwa  mujibu wa takwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).

No comments:

Post a Comment