NABII ELIYA - TUNAMJENGEA MCHIMBAJI MDOGO KESHO BORA, SIO BIASHARA TU - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, September 26, 2026

NABII ELIYA - TUNAMJENGEA MCHIMBAJI MDOGO KESHO BORA, SIO BIASHARA TU


NA MWANDISHI WETU GEITA


KATIKA siku iliyotengwa kwa ajili ya Wachimbaji Wadogo na Watoaji wa Msaada wa Kiufundi (TSA), Mkurugenzi wa Kampuni ya Nabii Eliya ameweka wazi falsafa ya kampuni yake ambayo imeibua matumaini mapya kwa wachimbaji.


Akizungumza kwenye Maonesho ya Tisa ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, mkurugenzi huyo alisema mafanikio yao hayapimwi kwa faida pekee, bali kwa namna wanavyowainua wachimbaji wadogo.


Amesema kwa muda mrefu wachimbaji wadogo wamekuwa wakikabiliwa na uzalishaji mdogo, gharama kubwa na ukosefu wa usalama kazini, changamoto ambazo kampuni yake imeamua kuzipatia suluhu za kudumu kupitia huduma za kiufundi.


"Lengo letu si biashara tu, ni kuinua mchimbaji mdogo. Tunapompa mchimbaji teknolojia sahihi, tunampa matumaini ya kesho iliyo bora kwa familia yake na jamii yake," alisisitiza.



Alifafanua kuwa mafanikio hayo yameonekana kupitia kuwawezesha vijana wa Kitanzania kupata ajira na ujuzi kwa vitendo migodini, kuleta teknolojia rafiki na nafuu inayolinda mazingira lakini kuongeza tija, pamoja na kurejesha kwa jamii kupitia miradi ya kijamii.


Maonesho hayo yanayoongozwa na kaulimbiu isemayo _"Kuwezesha Wachimbaji Wadogo, Kuongeza Tija, Kujenga Sekta Imara"_ yameendelea kuwa jukwaa muhimu la kutengeneza mwelekeo mpya wa sekta ya madini nchini.

No comments:

Post a Comment