PROF. SHEMDOE AKUTANA NA VIONGOZI WA MBINGA KUIMARISHA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, September 22, 2026

PROF. SHEMDOE AKUTANA NA VIONGOZI WA MBINGA KUIMARISHA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO


NA OWM – TAMISEMI


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, amefanya kikao kazi na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, wabunge na viongozi wa Wilaya ya Mbinga, kwa lengo la kujadili namna bora ya kuimarisha na kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Mbinga.


Kikao hicho kimejikita katika kujadili hatua na mikakati inayoweza kuchukuliwa ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya ya Mbinga inasimamiwa na kutekelezwa kwa ufanisi, kwa kuzingatia mahitaji na maslahi ya wananchi.


Kikao kazi hicho kimefanyika Septemba 22, 2026, katika Ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Magogoni ya Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, jijini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa pia na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini.







No comments:

Post a Comment