WAZIRI MKUU MWIGULU MGENI RASMI MKUTANO WA JUMUIYA YA KIISLAMU WAAHMADIYYA TANZANIA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, September 23, 2026

WAZIRI MKUU MWIGULU MGENI RASMI MKUTANO WA JUMUIYA YA KIISLAMU WAAHMADIYYA TANZANIA





NA MWANDISHI WETU

WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuwa mgezi rasmi katika Mkutano Mkuu wa Mwaka (Jalsa Salana) wa 55 wa Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya nchini utakaofanyika eneo Maarufu la Ahamdiyya liliopo Kitonga, Kata ya Msongola Wilayani Ilala jijiniDar es Salaam, Septemba 25 hadi 27 mwaka huu.


Akizungumza na wanahabari Septemba 22,2026 jijini humo, Amir na Mbashiri Mkuu Jumuiya hiyo Sheihk Khawaja Muzaffar Ahamad amesema utaratibu wa kufanyika mkutano huo ulianzishwa na  Mwanzilishi mtukufu wa jumuiya hiyo Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad.


Amesema mwanzilishi huyo alitumwa na Mwenyezi Mungu kuja kutimiliza bishara za ujjai wa Imam Mahdi pamoja na ujaji wa Masihi katika zama hizi zilivyobainishwa na Mtukufu Mtume Muhammad s.a.w na waanzilishi wa dini zingine duniani.


"Mkutano huu unafanyika ili kuongeza hofu ya Mwenyezi Mungu mioyoni mwa washiriki kupata Taqwa, kumjali Mungu, kuepukana  na mabaya, kupata moyo wa huruma na kuongeza upendo baina yao," amesema Sheikh Khawaja.


Amebainisha kuwa kwenye mkutano huo utahudhuriwa na viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, viongozi wa dini na viongozi wa kijamii kwa ujumla lengo likiwa kutoa nasaha zao.


Amesisitiza kuwa kauli ya Jalsa Salana ya maku ni Taqwa (uchamungu) ndio mzizi wa kila wema ikilenga kuwakaumbusha waumini juu ya ulazima wa kupata taqwa kwa kutekeleza maamrisho yote ya Mwenyezi Mungu na kujiepusha na makatazo yake yote, sio kwa lengo lolote bali kupata radhi na mapenzi ya Mungu tu.


Amefafanua kuwa mkutano huo utahudhuriwa na washiriki 5500 kutoka maeneo mbalimbali kutoka nchini na nje ya nchi na kwamba hotuba na nasaha za wataalamu wa jumuiya hiyo zitatolewa ikiwemo maisha  ya Mtume Muhammad s.a.w kuwa ni Chemchem ya Taqwa na uchamungu, jinsi ya maisha na mafundisho ya masihi na malezi bora ya familia pamoja na mafanikio katika maisha ya mtu.


Pia amesema washiriki wenye afya zao na rika linalorhusiwa watapata nafasi ya kuchangia damu kwenye Benki ya Taifa ya Damu Salama huku akikazia hotuba zote za Jalsa Salana ya mwaka huu zitasikika mubashara kupitia redio ya Ahmadiyya Mtwara na tovuti ya redio hiyo inayojulikana https: //www.radioahmadiyya.or.tz.


Sheihk Khawaja lengo la jumuiya hiyo ni kutangaza amani kwa ujumbe sahihi wa waislamu duniani kote na kuwa mstari wa mbele kupinga amani zisizo sahihi za mawazo zinazobainishwa na uislamu ikiwaemo jihadi ya upanga, ugaidi, kutokutii serikali zisizo za kiisalmu pamoja na kuwa misimamo mikali isiyovumilia wengine.

No comments:

Post a Comment