FM Academia kupiga shoo ya robo mwaka - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, October 19, 2011

FM Academia kupiga shoo ya robo mwaka

Na Eben-Ezery Mende
BENDI ya muziki wa dansi nchini, FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma' Oktoba 28 itafanya onesho la robo tatu ya mwaka ndani ya Ukumbi wa Hiltec Resort.
Mratibu wa onesho hilo, Sauda Mwilima alisema jana kuwa onesho hilo ameliandaa maalumu kwa ajili ya kuwakutanisha wapenzi wa muziki wa dansi na kuburudika huku wakitathmini mambo waliyoyafanya katika kukuza aina hiyo ya muziki kwa mwaka huu.
Alisema ikiwa imebakia miezi miwili mwaka 2011 kumalizika, wadau wa muziki wanatakiwa wakutane na kujadiliana kuhusu mambo waliyoyapanga kufanya katika kuboresha sekta hiyo na kuangalia walipofikia.
Mwilima alisema siku hiyo watahudhuria magwiji wa tasnia ya muziki wa dansi ambapo kabla ya kuanza burudani watapata muda wa kufanya mazungumzo kisha kufuatiwa na burudisho ya muziki kutoka kwa Wazee wa Ngwasuma.
Mbali ya FM Academia kutoa burudani siku hiyo, pia watatumia fursa hiyo kuwatambulisha waimbaji wa bendi hiyo wapya wanne wakiwemo wa kike wawili na wawili wa kiume.
Waimbaji hao wa kike ni Tombo Love na Bela Beloo na wa kiume ni Dispach Dock na Digital Foo.

Kiongozi wa bendi ya FM Acagdemia ,Nyoshi El Saadat

No comments:

Post a Comment