Manzabei yamkwangua Kassim mil 15/- - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, October 19, 2011

Manzabei yamkwangua Kassim mil 15/-

Na Geofrey Nanai
VIDEO ya wimbo wa 'Manzabei' wa msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Kassim Mganga umegharimu kiasi cha millioni 15/- hadi kukamilika kwake.
Akizungumza na Jambo Leo jijini Dar es Salaam jana kwa njia ya mtandao, Kassim alisema gharama imekuwa kubwa kutokana na viunga mbalimbali alivyotumia kurekodi video hiyo.
''Unajua video hii nimerekodi katika visiwa vya Unguja, Pemba na Tanga maeneo ya Manzabei, pia kuna helkopta mbili ambazo nilikodi ili kuifanya video hii kuwa ya kipekee,' 'alisema nyota huyo wa kibao cha Haiwezekani. 
Hata hivyo, Kassim alisema kuwalipa wacheza shoo, usafili, chakula na boti aliyoikodi vimechangia kuongezeka kwa gharama ya video hiyo, na baada ya mchakato mzima kukamilika itapelekwa kwenye vituo vya luninga. 
Aliongeza kuwa wimbo huo umetengenezwa katika studio za Visual Lab, chini ya mtayarishaji mahiri nchini, Adam Juma, na kudai kuwa kutokana na ubora wa wimbo huo anaamini kazi itakuwa ya kipekee na kuigwa.
Alisisitiza kuwa baada ya wimbo huo kuanza kuonekana katika vituo kadhaa vya luninga nchini, ataachia albamu yake mpya ya Tajiri Wa Mahaba.  

 

No comments:

Post a Comment