Islay Super Cup kupigwa Msasani - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, October 19, 2011

Islay Super Cup kupigwa Msasani

Na Salome Millinga
MICHUANO ya mpira wa miguu ya kuwania Kombe la Islay Super inatarajia kuanza Oktoba 22 mwaka huu katika Uwanja wa Magunia, Msasani jijini Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa mashindano hayo, Islay Mnyupe alisema kuwa mashindano hayo ambayo yatafanyika kwa mara ya kwanza mwaka huu yanatarajia kushirikisha timu 16.
Alisema kuwa ada ya kushiriki katika mashindano hayo ni sh 10,000, ambapo pia, timu mbalimbali zimeshachukua fomu kwa ajili ya kindumbwendumbwe hicho. Hata hivyo, utaratibu wake unaweza kubadilika ikiwa zitajitokeza timu zaidi.
Alisema wameanzisha mashindano hayo kwa ajili ya kukuza kiwango cha soka ikiwa ni pamoja na kuwakinga vijana na maambukizi ya UKIMWI pamoja na utumiaji wa dawa za kulevya.
Mkurugenzi huyo aliongeza: "Mshindi wa kwanza atapata mil 1.2/-, mipira miwili pamoja na kombe, wa pili atapata sh 500,000, na mwamuzi pamoja na mchezaji bora watapewa sh. 50,000 kila mmoja.
"Nimeandaa mashindano kwa mara ya kwanza na yanatarajia kuvuta hisia za mashabiki wengi kutokana na ujumbe tuliokujanao, na yatakuwa na msisimko mkubwa kwani maandalizi yake yameshakamilika."
Alizitaja baadhi ya timu zitakazoshiriki kuwa ni pamoja na Mawingu, Black People, Voice Of Lion, Castro FC, Super Boys, Ubanda, Kumbukumbu, AMREF FC, Nyara FC na Marketing ambazo zimeshachukua fomu.

No comments:

Post a Comment