Hamisi Magendela
KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya golf, Farayi Chitengwa, amesema mashindano ya Afrika Mashariki yanatarajiwa kufanyika nchini Novemba 7, huku wachezaji wake wakiwa katika mazoezi makali.
Akizungumza na Jambo Leo Dar es Salaam jana, Chitengwa alisema timu yake iko katika maandalizi mazuri kuhakikisha ubingwa unabaki nchini msimu huu wakitumia uenyeji wao.
"Vijana wangu wako katika maandalizi mazuri ya kujiandaa na mashindano hayo, na sasa wachezaji wamechaguliwa vijana 12 ambapo kabla ya kuanza kwa mashindano watachujwa na kubaki wanne," alisema Chitengwa.
Alisema kabla ya mashindano hayo kuanza, kutakuwa na mashindano mengine yanayotarajiwa kuwa sehemu ya kuchuja wachezaji watakaoiwakisha nchi yajulikanayo kama Dar Open.
Chitengwa, alisema mashindano hayo yatashirikisha washiriki kutoka mikoa mbalimbali na yatafanyika Oktoba 29 mwaka huu katika Viwanja vya Lugalo, yakitumika kama maandalizi ya michuano ya Afrika Mashariki na Kati.
Alisema mashindano ya Dar Open yatakuwa ya siku mbili, na watayatumia ipasavyo kupata wachezaji wenye viwango watakaoiwakilisha nchi katika mashindano ya Afrika Mashariki mwezi ujao.
Wednesday, October 19, 2011
New
Chitengwa aongeza kasi maandalizi ya gofu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment