Na Hamisi Magendela
TIMU ya soka ya Coastal Union ya Tanga 'Wagosi wa Kaya' inaendelea na mazoezi ya kujiimarisha katika harakati zao za kujiondoa mkiani mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu.
Akizungumza na Jambo Leo Dar es Salaam jana, Mwentekiti wa Coastal, Mohamed Aurola, amesema kikosi chake kinaendelea vizuri licha ya mchezaji mmoja kuwa majeruhi.
"Nashukuru wachezaji wangu wako katika hali nzuri na wametuahidi kufanya vizuri katika michezo iliyobakia kabla ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza, tunataka kumaliza tukiwa hatuko mkiani," alisema.
Alisema kipigo walichokitoa kwa timu ya Villa Squad ndiyo dozi itakayoendelezwa kwa timu nyingine watakazokutana nazo katika michezo hii ya mzunguko wa kwanza.
Siku chache zilizopita, timu hiyo iliibuka na ushindi mnono wa mabao 6-1 dhidi ya Villa Squad, katika mchezo uliokuwa wa upande mmoja na kusababaisha Villa kuwasimamisha baadhi ya wachezaji wao.
Wednesday, October 19, 2011
New
Villa waipa kiburi Coastal Union
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment