Miss Uhuru 2011 yaja - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, October 19, 2011

Miss Uhuru 2011 yaja

Na Ashura Ally
MASHINDANO ya kumtafuta Miss Uhuru yanatarajiwa kufanyika Desemba  8 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Akizungunza Dare es Salaam jana, Mkurugenzi wa Masoko wa Rush - Way International, Dominick Haule, alisema lengo la mashindano hayo ni kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru, itakayofikia kilele chake Desemba 9.
"Kama ilivyo katika kumbukumbu zetu kwamba mwaka huu Tanzania itaadhimisha miaka 50 ya Uhuru, kwa umuhimu wa siku hiyo, Rush way imeamua kubuni na kuandaa shindano la urembo linalofanana na maudhui ya  siku ya Uhuru na kuliita 'Miss Uhuru'," alisema Haule.

Haule alisema  mashindano hayo kitaifa yatafikia kilele chake kila usiku wa Desemba 9 kila mwaka kuanzia mwaka huu.
Kwa mwaka huu, shindano hilo litachukua majuma sita, na mawakala wataendesha mashindano kwa muda wa majuma manne, na Miss Uhuru Taifa wataendesha kambiya majuma mawili.
Pia, alisema walengwa au washiriki  ni wasichana wote wa Kitanzania kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara ambao wana umri wa mika18 na usiozidi miaka 25, elimu kuanzia kidato cha nne na kuendelea, tabia njema, uwezo binafsi wa kufikiri, uwezo wa kulinda na kutetea utu wa Mtanzania hususani mwanamke ni kati ya sifa zitakazoangaliwa.
Hata hivyo, alisema washiriki wote watapewa mafunzo mbalimbali ya historia ambayo yana hazina na kumbukumbu mbalimbali za taifa, na mshindi wa Miss Uhuru Taifa atazawadiwa gari aina ya Vitara. 

No comments:

Post a Comment