Five yaenda kusini kutambulisha albamu - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, November 21, 2011

Five yaenda kusini kutambulisha albamu

Na Hamisi Magendela
KUNDI la mwambao Five Star 'Watoto wa Bongo'
wanaondoka kwenda mikoa ya kusini kwa ajili ya
kutambulisha albamu yao ya 'Mwenye Hila
Habebeki'.
Akizungumza na Jambo Leo Dar es Salaam jana
Rais wa kundi hilo Alli Juma 'Alli Jay'
wanaondoka leo na kutaraji kurudi Novemba 29
mwaka huu.


"Tuko kamili kwa ajili ya kutoa buudani kwa
wapenzi wetu wa kusini ya Lindi na Mtwara,
hivyo tunaamini mashabiki wa mikoa hiyo
watatupokea kwa mikono miwili," alisema Alli
Jay.
Alisema  wakirejea kutoka mikoa hiyo ya kusini
watafanya onesho moja katika ukumbi wa Burhega
Tekeme kabla ya kwenda mikoa ya nyanda ya
ziwa.
Aliongeza kuwa katika onesho hilo watapanda
jukaa moja na msanii chipukizi wa muziki wa
kizazi kipya Asley anaetamba na 'Nakusemea kwa
Mama'kinachpfanya vizuri katika vituo vya
redio na luninga.

Stars ya pooltable yarejea,mashindano
yaahirishwa
Na Hamisi Magendela
TIMU ya mchezo wa pooltable iliyoondoka
Novemba 16 kwenda Malawi kwa ajili ya
mashindano ya Afrika imerejea nchini baada ya
mashindano hayo kufutwa.
Akizungumza na Jambo Leo Dar es Salaam jana
Katibu Mkuu wa chama cha mchezo huo Tanzania
(TAPA) Amosi Kafwinga, alisema mashindano hayo
yalifutwa kutokana na tatizo la kisiasa
lililopo nchini humo.
"Kutokana na tatizo la kisiasa lililopo Malawi
kwa sasa Baraza la vyama vya mchezo huo Afrika
,limeamua kuyafuta mashindano hayo hadi
yatakapotangazwa tena," alisema Kafwinga.
Alisema kwa sasa timu hiyo inacheza michezo ya
kirafiki katika Mikoa ya Manyara, Arusha
Kilimanjaro, Tanga baada ya ziara hiyo
kumalizika wanatarajia kurejea Dar es Salaam
Novemba 25 mwaka huu.
Timu hiyo iliondoka Novemba 16 mwaka kwenda
nchini Malawi kushiriki mashindano hayo ya
Afrika lakini kutokana na sababu za kisiasa
yamefutwa kutokana na usalama wa washiriki wa
mashindano hayo kuwa mdogo.


Na Hamisi Magendela
BAADHI ya wanamuziki wa kundi la kizazi kipya
Mexicana Lacavela wamekanusha habari za
mkataba wao kuisha kwenye kundi hilo.
Akizungumza na Jambo baadhi ya wasanii
waanzilishi wa kundi hilo Stayharm Milanzi
'Climax Bibo' alisema  Praygod Kweka Baghdad
hana jukumu la kutoa maelezo hayo.
"Baghdad alilikuta kundi letu likiwa tayari
limeshaundwa, sijui yeye kama nani katika
kundi letu kwani hata kwenye uwanzishwaji
hakuwepo," alisema Climax Bibo.
Climax, alisema Baghdad alipewa madaraka ya
usambazaji wa kazi za kundi hilo kutokana na
uwezo wake wa kufanya hivyo.
Pia Edward Paul 'Fidodido', alisema tangu
ajiunge na kundi hilo hakuelezwa juu ya
mikataba ya kundi, hivyo suala la kusaini kwa
mikataba mipya ili kuweza kuendela na kundi
hilo halina ukweli wowote.
Baghdad ambaye anadai ni kiongozi wa kundi
hilo, alisema wasanii waliomo kwenye kundi
wanatakiwa kusaini mikataba mipya ili waweze
kuendelea kuwemo kwenye kikosi chake.

No comments:

Post a Comment