Villa kuingia kambini kesho
Na Asmah Mokiwa
TIMU ya soka ya Villa Squad kuingia kambini Desemba 19 mwaka huu ili kujiweka sawa na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya soka Tanzania bara inayotarajia kuanza mapema Januari, mwakani.
Akizungumza Dar es Salaam jana Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo, Ramandani Sudi alisema wachezaji wake tayari wameshaanza mazoezi ya kawaida kusubiri wachezaji wawili ambao bado hawajawasili.
Alisema hao ni wale waliosajiliwa kwenye dilisha dogo la usajili kutoka mikoani na ikiwa hawajawasili hadi leo wataingia kambini kuanza na harakati za kumaliza ligi Ligi wakiwa katika nafasi nzuri na kuepuka hatari ya kushuka daraja.
"Licha ya kufanya vibaya katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu bado tunaimani na timu yetu kufanya vyema katika mzunguko wa pili na hatimae timu inasonga mbele" alisema Sudi.
Alisema watafanya jitihada kuhakikisha hawashuki daraja msimu huu na badala yake kujiweka katika nafasi za juu katika ligi.
Saturday, December 17, 2011
New
Villa kuingia kambini kesho
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




No comments:
Post a Comment