Na Asmah Mokiwa
FAMILIA ya masumbwi nchini imekubwa na msiba mzito wa Bondia wa ngumi za kulipwa, Mohammed Kidevu.
Bondia huyo amefikiwa na umauti juzi usiku baada ya kukanyagwa na roli la mchanga baada ya kutereza wakati akipanda roli hilo kwa nyuma.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kocha Msaidizi wa ngumi Mkoa wa Ilala, Ramadhani Mhamila (Super D) alisema bondia huyo alifikwa na umauti akiwa katika shughuli zake za kuchimba mchanga Dondwe, Chanika, Dar es Salaam.
"Baada ya kumaliza shughuli zake alidandia roli hilo kwa nyuma kwa madhumuni ya kupanda lakini alitereza na kumkanyaga kwa nyuma na kufariki dunia,"alisema Super D.
Kwa mujibu wa Super D alisema mwili wa marehemu huyo umehifdhiwa katika hospitali ya Amana, Dar es Salaam wakati taratibu za mazishi zinafanywa.
Saturday, December 17, 2011
New
Bondia afariki dunia
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




No comments:
Post a Comment