-Wakoloni walididimiza Sanaa yetu
-Awatataka wasanii kuwa wabunifu
Na Hamisi Magendela
BAKARI Mbelemba ni miongoni mwa wabobezi wa sanaa za maigizo nchini wanaofanya vizuri na kuwa kama sehemu ya mgodi wa almasi kutokana na vitu adimu alivyokuwa navyo.
Anafahamika zaidi kwa jina la Mzee Jangala, sina shaka wadau mbalimbali watakubalina nami kuwa nguli huyo ni baadhi ya madini yaliyobaki katika tasnia ya sanaa za maigizo nchini.
Mzee Jangala anasema alianza masuala ya sanaa za maigizo mwaka 1975 baada ya kupata mafunzo sanaa ya miaka miwili yaliyokuwa yakitolewa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo wakati huo na kumpa mwanga katika suala zima la Sanaa.
Anasema baada ya hapo aliajiwa na hiyo mwaka 1977 kwa ajili ya shughuli za kuendeleza sanaa nchini ambazo kwa wakati huo ilikuwa ikionekana kuwa na nguvu kubwa kutokana na kuzingatia maadali tofauti na ilivyo sasa.
Pia anasema wakati huo ikijitoka kundi ambalo linavunja maadali vyombo husika havikusita kuchukua hatua madhubuti ikiwemo kulifungia kundi hilo kuendelea na sanaa nchini lakini
kwa sasa hali imekuwa ni tofauti.
Anasema aliingia Radio Tanzania wakati huo ikiitwa RTD, sasa Taifa akiwa mtunzi wa mashahili kabla ya kampuni ya Chibuku kuingia naye mkataba wa kutoa elimu mbalimbali
kupitia michezo ya kuigiza kupitia radio.
Mzee Jangala anaweka wazi kuwa hapo ndipo akaanza rasmi kucheza michezo hiyo kwenye radio ambayo iliweza kumpa umaharufu mkubwa japo maslahi yake yalikuwa madogo kwa
wakati huo.
Nyota huyo wa sanaa za maigizo anasema wakati anaingia kwenye tasnia hiyo maadili yalikuwa yakizingatiwa kwa nguvu zote na yalikuwa yanatoa mafunzo kwenye jamii ambayo wengi
wao walikuwa wakielimika kupitia sanaa hiyo.
Anasema kwa sasa sanaa imekuwa ni biashara ambayo inawangizia kipato wasanii na kusababisha maadili kupolomoka siku hadi siku kitu ambacho kinatakiwa kufanyiwa kazi mapema.
Mzee Jangala anasema fani ya sanaa za maigizo zilialibiwa na wakoloni wakiwa na lengo la kutimiza haja zao za kutawala, hivyo kwa njia moja au nyingine baadhi ya watu waliweza kuhathirika na hilo.
Nguli anasema baada ya sanaa kuoneka kuzidi kudidimia Mwalimu Nyelele akasema Taifa lisilokuwa na utamaduni wake ni sawa mwili usiokuwa na moyo.
Afafanua kuwa baada ya kauli hiyo ya Mwalimu Masharika
mbalimbali yaliibuka na kuanzisha vikundi vya sanaa bila kuangalia wanaojua misingi ya sanaa asiliahali iliyosabisha pia kuharibu zaidi.
Bobezi huyo wa sanaa za maigizo nchini anasema jitihada zinahitajika kwa wasanii kuongeza ubunifu wa kazi zao ili kutengeneza kazi zenye ubora zaidi na siyo kila siku kuigana kusikokuwa na sababu za msingi.
Anasema kwa sasa sanaa inatumika bila kulatibiwa hali inayosababisha kupoteza mvuto kwa mashabiki, hivyo anasema nik vyema ikaendeshwa kwa kurabitiwa ili nembo ya Taifa ibaki palepale.
"Wasanii siku zote wanatakiwa kuumiza vichwa ili kutengeza kazi nzuri zitakazowanya kuwa wapya kila siku na mashabiki kuwa na hamu ya kufuatailia kazi nyingine ya msanii wakiamini kuwa kutakuwa na utofauti na nyingine," anasema Mzee Jangala.
Nguli huyo wa sanaa za maigizo nchini wakati akiendelea na shughuli hizo mwaka 1980 alipata kazi ya kufundisha sanaa katika chuo cha sanaa bagamoyo kabla ya kuacha kazi hiyo mwaka 1984.
Baada ya kuacha kazi ya kufundisha katika chuo cha sanaa Bagamoyo alianza kufanya shughuli mbalimbali za tafiti juu ya suala zima la kuendeleza fani hiyo nchini ambayo kwa sasa imekuwa na utofauti mkubwa na zamani.
Anasema licha ya kufanya tafiti mbalimbali juu ya sanaa nchini pia aliweza kufanya shughuli za kuendeleza fani hiyo katika vikundi mbalimbali ambavyo kwa wakati huo vilikuwa vikifanya vizuri na kuipua vipaji vya wasanii lukuki.
Mwaka 1989 aliamua kuanzisha kikundi chake binafsi ambacho hadi leo bado kinaendelea na shughuli sanaa cha Mandela Theatre kikiwa ni moja ya vikundi chache vilivyosimama hadi
leo.
Mkongwe huyo wa sanaa nchni nchini anasema changamoto kubwa anazokutana nazo ni pamoja kufikiri na kundaa vitu ambavyo vitasimama muda mrefu katika medani ya sanaa za maigizo nchini.
"Unajua mara nyingi huwa naumiza kichwa kutafuta kitu ambacho kitavuta mashabiki wengi na kuwa bora ambacho kitalinda maadili ya Mtanzania popote kazi inaposikilizwa bila kubagua umri," alisema Mzee Jangala.
Anasema ili wasanii waweze kufanya vizuri ni vyema wakaenda shule kusoma sanaa baada ya kufanya kwa mazoea kwa maana siku zote shule ina umuhimu wake katika jambo lolote, uwezi kuwa Daktari mzuri bila ya kwenda shule ndivyo ilivyo kwenye sanaa pia.
Anasema kupitia sanaa ameweza kupata maraifi ndni na nje ya nchi, kupata nafasi ya kwenda nchi mbalimbali ikiwemo Nigeria, Zambia, Finland, Swiden na nyinginezo.
Mzee Jangala anasema amezaliwa July 5, 1950 Luhoi wilayani
Rufiji mkoani Pwani hadi sasa na amefanikiwa kuwa na watoto
wawili ambao bado wanaendelea na masomo.
Bobezi huo katika shughuli sanaa za maigizo nchini ambaye pia ni mtoto watatu katika ya wanne wa mzee Kassim Mbelemba anasema elimu yake ya alipata katika shule ya Mkura iliyopo
Kilombero mkoani Morogoro wakati middle school alisoma katika shuke ya Igota iliyopo Ulanga na kuhitimu kidato cha nne
mwaka 1973.
Anasema kwa sasa anafikiria kuanzisha kituo cha sanaa zote ili waweze kutanuana mawazo ili kuwaweza kuendeleza fani hiyo.
"Tayari limeshapata eneo la kujenga kituo hicho na kwa sasa nipo kwenye harakati za kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho," anasema Jangala.Pia anasema kutokana na mashabiki wengi kuona kazi zake kwenye Luninga wako katika hatua za mwisho kukamilisha suala hilo, hivyo wadau mbalimbali wakae tayari kuwapokea kupitia Luninga baada ya mchakato huo kukamilika.
Akimzungumzia Mzee Kipara, Jangala alisema kwamba atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa wa kukuza na kuibua wasanii wengi katika tasnia hiyo na pia kutokuwa mchoyo wa kugawa ujuzi wake.
“Binafsi nilifanya naye kazi Redio Tanzania wakatio huo ikiitwa RTD sasa TBC Taifa, tukiwa katika vitengo viwili tofauti.
“Yeye alikuwa upande wa maigizo ya redio akiwa analipwa na redio hiyo moja kwa moja, mimi nilikuwa upande wa maigizo ya biashara.
Hivyo namfahamu vya kutosha,” anasema. Mzee Jangala hakusita kutoa wito kwa wasanii wa maigizo
kuenzi mchango wa Mzee Kipara kwa kuendeleza na kudumisha fani ya maigizo pamoja na kuongeza ubunifu.
0718594040
James Michael Kibosho:
Mkali wa drums anayeing'arisha Twanga Pepeta
- AAlimshangaza lly Choki kwa uwezo wake
- Ni mwanafunzi wa Petit Makambo
Na Hamisi Magendela
"NILIANZA kuchezo shoo katika kumbi mbalimbali za starehe na kwenye shughuli ikiwemo maharusi kabla ya kuingia kwenye kupiga 'drums' ambayo ndiyo ilikuwa ndoto yangu kubwa maishani mwangu".
Ndivyo alivyoanza kujieleza mpiga vyombo huyo tegemeo wa bendi ya muziki wa dansi ya African Stars 'Twanga Pepeta', James Michael akijulikana na wengi kwa jina la 'Kibosho', ambalo ni jina la ukoo wao.
Mwanamuziki huyo ambaye kwa sasa anabeba jahazi katika upande wa kucharaza mabati hayo, ambayo yanakuwa ni muongozo kwenye upigaji wa vyombo, anasema anajisikia faraja kufikia hatua hiyo baada ya kutoka kwenye safari ndefu.
Nyota huyo ambaye ni mtoto wa tano katika kuzaliwa, kati ya watoto watano wa mzee Michael, anasema baada ya kumaliza elimu ya msingi 2001, katika shule ya msingi Umoja iliyopo Mabibo, Dar es Salaam, Manispaa ya Kinondoni, na kuingia rasmi kwenye tasnia hiyo.
Anasema 2002 alianza kujifunza kupiga 'drums' katika bendi ya Lolita, na kutokana na kuwa na kiu ya kupenda fani hiyo aliweza kujua kwa haraka na kuanza kupiga katika bendi zilizokuwa zikipiga muziki kwenye kumbi kwa ujira wa sh 1500 hadi 2000 kwa siku.
"Kupiga drums katika bendi hizo nilipata ujuzi wa kutosha na kufanikiwa kujiunga katika bendi ya Maliki Star iliyokuwa ikiongozwa na Petit Makambo, ambaye alinipa mafunzo zaidi ya kutumia chombo hicho ambacho sasa napata riziki.
"Kwa kweli alinipa siri kubwa ambayo hadi naitumia kuwa tofauti na wapiga 'drums' wengine, na hadi leo namheshimu sana," alisema J Kibosho.
Anasema baada ya kipindi kifupi, alikwenda Jijini Tanga kuanzisha bendi ya Super Sound, nayo ilikuwa chini ya Makambo.
Mapema 2003, wakaenda Dar es Salaam kurekodi nyimbo kadhaa ambazo zilikuwa zimekamilika baada ya kukaa kambini Jijini Tanga kwa muda wa miezi sita.
Anabainisha kuwa baada ya kumaliza kurekodi nyimbo mbalimbali, walirejea Jijini Tanga, ndipo akasikia kuwa bendi mpya inayoitwa Extra Bongo ikiwa chini ya 'Mzee wa Farasi', Alli Choki, ndipo akapata ushawishi wa kwenda Dar es Salaam kujaribu bahati yake.
"Ilikuwa kawaida yangu kujaribu kila eneo nililohisi kuwa na mafanikio japo ilikuwa kawaida yangu kununua kanda za kaseti na kusikiliza na kuzifanyia mazoezi, kitu ambacho kiliniwezesha kujua mapigo ya nyimbo mbalimbali tofauti," anaweka wazi Kibosho.
Mwanamuzki huyo anasema aliweza kununua kaseti ya albamu ya Extra Bongo ya 3X3 kwa lengo la kupata uzoefu kabla ya kwenda Dar es Salaam kujaribu bahati yake.
Baada ya kufanya mazoezi ya kutosha na kujiridhisha kuwa amefikia kiwango cha kutosha, alinyanyua mguu nakwenda Dar es Salaam na kuomba nafasi ya kujaribiwa kupiga kifaa hicho.
"Nilikutana na Mkurugenzi wa bendi, Choki, baada ya kuzungumza naye alinijaribu kupiga drums kwa hakika nilifanya 'wonders', kila mmoja alikubali uwezo wangu baada ya kupiga kibao cha 3X3," alisema J Kibosho.
Anasema baada ya miezi mitatu aliitwa na uongozi wa bendi hiyo na kutambulishwa rasmi kupigia bendi ya Extra Bongo.
"Nilijisikia faraja kuwemo katika kikosi kazi cha bendi hiyo nikiamini kuwa ulikuwa mwanzo wa kuonekana kuelekea kwenye mafanikio kupitia tasnia hiyo," anasema.
Mwanamuziki huyo aliyezaliwa Desemba 17, 1987 Jijini Dar es Salaam, anasema baada ya kuingia katika bendi hiyo, alifanikiwa kupiga nyimbo kadhaa ikiwemo ya Duble Duble iliyofanya vizuri katika maeneo mbalimbali, na baada ya siku chache kundi hilo lilivunjika na kujiunga Double Extra iliyokuwa chini ya Mwinjuma Muuni na Alli Choki 'Mzee wa Farasi' na kwenda Chalinze kukaa kwa miezi miwili kabla ya kutoa albamu ya kwanza iliyopewa jina la Chungeni Ndoa.
2004, bendi hiyo ilivunjika na kujiunga na bendi ya Double M Sound akiwa chini ya Muumini 'Kocha wa Dunia', na wakafanikiwa kutoa albamu ya Titanic iliyokuwa na nyimbo saba, na kufanikiwa kupiga nyimbo sita ikiwemo Ukewenza, Titanic, Ndoa ya Ufukara, Mapenzi Siyo Mtaji, Air Omani ambayo haikufanya vizuri katika soko la muziki.
"Unajua kutokana na matatizo madogo, bendi ilivunjika, nikajiunga na Mchinga Sound 'G8' ambayo nilidumu kwa wiki moja tu, ndipo nikapata nafasi ya kujiunga African Stars 'Twanga Pepeta' na kupokelewa na Choki, Mzee Wa Farasi baada ya kufaulu kupiga vyema kibao cha Safari 2005," anasema.
Mpiga drams wa African Stars 'Twanga Pepeta' James Kibosho akiwajibika jukwaani.
"Tangu 2006 nilipotua nimeweza kushiriki kupiga albamu zote na 2008 aliniachia nyimbo 5 kati ya 7 ya albamu ya Sumu Ya Mapenzi.
"Kwa kweli Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Abuu Semhando, hakika bado namkumbuka kutokana na mchango wake kwangu kwa jinsi alivyokuwa akinishauri na kunipa muongozo ambao unanipa mwelekeo mzuri katika fani hii," anasema Kibosho ambaye ni mdogo wa mpiga 'drums' wa bendi ya Extra bongo, Martine Kibosho.
Kibosho anavutiwa zaidi na mpiga 'drums', Peter Col wa Werrason Ngiama ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na malengo yake ni kuanzisha bendi yake mwenyewe.




No comments:
Post a Comment