- MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, May 19, 2012

Ni Twiga Stars vs Banyana Banyana U/Taifa leo
Na Asha Kigundula
TIMU ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) leo itashuka dimbani kuvaana na timu ya Taifa ya wanawake ya Afrika Kusini (Banyana Banyana) mechi itakayofanyika kwenye Uwanja wa taifa Dar er Salaam.
Mechi hiyo ya kirafiki ambayo itafanyika kesho kuanzia saa 10, alasiri.
Twiga Stars inacheza mechi hiyo kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Ethiopia.
Mechi dhidi ya Ethiopia itachezwa Mei 27 mwaka huu jijini Addis Ababa
 Banyana Banyana iko katika kinyang’anyiro cha kutafuta tiketi ya Fainali za AWC ambapo katika raundi hii ya pili imepangiwa Zambia na itaanzia mechi hiyo ugenini jijini Lusaka.
Wakizungumzia mchezo huo makocha wa timun hizo mbili Boniface Mkwasa wa Twiga Stars na Joseph Mkhonza wa Banyana Banyana, walisema wamejipanga kupanga vikosi vyao ambavyo vitacheza mechi zao zijazo.
Mkwasa alisema mechi hiyo itasaidia kuwaweka wachezaji qwake katika hali nzuri kabla ya mchezo wao huo ujao.
Alisema wanaifahamu Banyana Banya kuwa ni timu nzuri hivyo kipimo cha mchezo huo kitasaidia kuipa hali kubwa timu yao.
"Nina uhakika mchezo huo ni kipimo tosha kwa timu yangu na wachezaji wangu ambao watacheza mechi ijayo dhidi ya timu ya Taifa ya Ethiopia"alisema Mkwasa.
Naye Mkhonza alisema anaijua vizuri Twiga ana imani ni kipimo tosha kwa timu yake kabla ya kwenda Zambia katika mchezo huo.
Alisema wachezaji wake wapo tayari kucheza na Twiga na timu ya taifa ya Zambia ambayo ni mechi muhimu sana kwao kushinda ugenini.
Twiga Stars na Banyana Banyana zote ziko katika raundi ya mwisho ya AWC ambapo zikifanikiwa kuwatoa wapinzani wao zitakwenda kwenye fainali hizo zitakazofanyika Novemba mwaka huu nchini Equatorial Guinea.
cioo

Na Hamisi Magendela

ALIYEKUWA kiungo mkabaji wa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba, marehmu Patrick Mafisango, atazikwa leo mjini kinshasa nchini Congo.
Mafasango aliyefariki dunia Mei 17 mwaka huu, kwa ajali ya gari iliyotokea Keko Dar es Salaam, anazikwa leo Mjini Kinshasa, Congo DRC.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa wakati mwili wa marehemu Mafisango aliyezaliwa mwaka 1980 ukiagwa katika viwanja vya Sigara Dar es Salaam juzi, zilisema marehemu atasafirishwa (kesho) jana kwenda DRC kwa maziko.
Mwili wa Mafisango ulisafirishwa jana alfajiri kwa Shirika la Ndege la Kenya (KQ) na kuwasili asubuhi ya saa tano na kupokelewa na wadau mbalimbali nchini Congo DRC na kuzikwa leo kwa wazazi wake mjini Kinshasa.
Wakati wa kutoa hotuba fupi katika viwanja vya Sigara, uongozi wa klabu ya Simba ulisema ili kuenzi jezi namba (30) iliyokuwa ikitumiwa na marehemu Mafisango  inasitisha kuitumia wakiwa na maana kama amestaafu.
"Tumeamua kuacha kuitumia jezi namba 30 iliyokuwa ikitumiwa na Mafisango kwa kuwa ndiyo kama amestaafu kwa lengo la kuthamini mchango wake wakati anaitumiaka klabu yetu," alisema Kaburu.
Mafisango aliyekuwa na uraia wa Rwanda mwenye asili ya Congo DRC enzi za uhai wake licha ya kuichezea timu ya Taifa ya Rwanda 'Amavubi' pia aliwahi kuzitumikia timu mbalimbali zikiwemo TP Mazembe ya Congo, APR ya Rwanda aliyocheza pamoja na Boniface Pawassa sambamba na Haruna Niyonzima, Azam FC na kujiunga na Simba hadi mauti ulipomkuta.
Kiongozi wa msafara katika mazishi ya marehemu Mafisango kwa upande wa klabu ya Simba umewakilishwa na Joseph Itang'ale 'Mzee Kinesi' na Haruna Moshi Boban ni miongoni mwa waliojumuika katika safari hiyo.
Marehemu ameacha watoto watatu, Mungu ailaze roho yake mahala pema Peponi. Amini.
cioo

Yanga yasogeza mbele kikao na wazee
Na Asha Kigundula
KAMATI ya utendaji ya klabu ya Yanga imesogeza mbele kikao maalum na Wazee wa klabu hiyo kilichokuwa kifanyike leo.
Akizungumza Dar es Salaam jana Ofisa habari wa Yanga, Louis Sendeu, alisema katika kikao cha kamati ya utendaji kilichofanyika hivi karibuni kimeamua kusogeza mbele mpaka itakapokaa na kupitia mapendekezo ya aliyekuwa mfadhili wa klabu huyi Yusuph Manji.
Sendeu alisema kuna maelekezo mfadhili huyo ametoa hivyo kamati ya utendaji imeamua kuyafanyia kazi na kuamua kusogeza mbele kikao hicho.
Alisema tarehe ya kikao hicho itapangwa tena kutokana na suala hilo ambalo linatakiwa kukaa chini na kuangalia maelekezo hayo.
Sendeu alisema mfadhili huyo ametoa mapendekezo yake ambayo yanafanyiwa kazi.
"Kamati ya Utendaji ilikutana na kuamua kusogeza mbele kikao cha Wazee kutokana na kuyafanyia kazi mapendekezo ya Manji ambaye anataka kurudi kudhamini klabu hiyo"alisema Sendeu.
Hata hivyo Sendeu alifafanua kuwa kuna kauli zinatolewa kuwa kikao hicho kilikuwa nalengo la kumuondoa mwenyekiti wa klabu hiyo Lloyd Nchunga ambapo si

Yanga iliyoingia katika mgogoro mkubwa ilikuwa ifanye kikao chake leo na wazee huku mwezi Julai 15 ikiwa imepanga kufanya Mkutano Mkuu wa mwaka wa klabu hiyo.
mwishio

No comments:

Post a Comment