Na Mwandishi Wetu
FAINALI ya mashindano ya mpira wa miguu ya Ester Cup inatarajiwa kutimua vumbi leo katika Uwanja wa Sabasaba, Bunda mkoani Mara.
Kwa mujibu wa Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mkoa wa Mara, Ester Bulaya timu ya Elimu Fc na Bunda Sport zitamenyana ili kumpata mshindi ambaye atajinyakulia kitita cha sh. milioni moja.
Bulaya alisema mshindi wa pili atajipatia kiasi cha sh. 500,000 huku mshindi watatu akijipatia kitita cha sh. 300,000.
Alisema zawadi nyingine ni sh.100,000 kwa timu yenye nidhamu , golikipa bora sh.50,000 huku mfungaji bora akinyakua sh.50,000.
Mashindano ya Ester Cup ambayo yameasisiwa, kudhaminiwa na kuratibiwa na mbunge huyo lengo lake ni kukuza michezo wilayani humo na mkoa mzima wa Mara.




No comments:
Post a Comment