Miss Tanga yaanza kunoga - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, May 3, 2013

Miss Tanga yaanza kunoga


Na  Mwandishi wetu

MAZOEZI kwa ajili ya kujiandaa na shindano la kumsaka malkia wa Mkoa wa Tanga mwaka huu "Redd's Miss Tanga 2013" yanatarajia kuanza Jumatano Mei 8 kwenye Ukumbi wa Lavida uliopo jijini Tanga.
Akizungumza na gazeti hili jana Mkurugezi wa Kampuni ya Datk Entertainment inayoratibu shindano hilo, Asha Kigundula   alisema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri.
Kigundula alisema kuwa walimu watakaosimamia warembo hao ni Miss Tanga 2012, Teresia Kimolo na Miss Tanga 2011, Zubeda Seif.
Alisema  warembo wameanza kuitikia wito wa kushirikishi shindano hilo ambapo mpaka sasa warembo nane wamejitokeza  na kuongeza nafasi  bado iko wazi kwa wasichana wote wenye sifa za kushiriki.
"Kila kitu kinaendelea vizuri, ikiwa na warembo kuendelea kujiandikisha kushiriki shindano la mwaka huu, ambalo nina hakika litakuwa la aina yake," alisema Kigundula
Alisema shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo mkoani humo kwa kuwa Kampuni ya Datk imejipanga, hivyo mashabiki wa mashindano ya urembo wa Tanga wakae mkao wa kupata raha.
Pia alisema fomu zinapatika katika ofisi ya Mwananchi iliyopo Bandari Tanga ghorofa ya nne, Five Brothers kwa Nassa Makau iliyopo jijini humo, kwa Dar es Salaam zinapatikana katika ofisi za Jambo Leo zilizopo Jengo la Hifadhi House zilizopo Posta.

No comments:

Post a Comment