Simiyu wapongeza ubingwa Yanga - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, May 3, 2013

Simiyu wapongeza ubingwa Yanga


Na Mwandishi Wetu
WANACHAMA wa Yanga tawi la Simiyu mkoani humo wameipongeza timu yao kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara 2012-2013, lakini wameushauri uongozi kufanya usajili makini kwa ajili ya msimu ujao na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga imetwaa ubingwa wa Bara huku ikiwa na mechi mbili mkononi, ambapo sasa imebakiza mechi  moja dhidi ya wapinzani wao wa jadi Simba Mei 18, mwaka huu na lengo lao ni kushinda ili kunogesha ubingwa wao.

Akizungumza kwa simu jana kutoka mkoani Simiyu
msemaji wa tawi la Simiyu, Ramadhan Kihamia alisema
wanachama wapatao 700 wameipongeza timu hiyo kwa kutwaa ubingwa, hivyo wameushauri uongozi ujipange imara kwa ajili ya ligi ya mabingwa hapo mwakani.

"Safari hii tunataka kuona klabu yetu inaandika historia kubwa katika michuano ya Ligi yaMabingwa Afrika, hatutaki kila siku kuishia kwenye ubingwa wa Bara tu, iwe mwendelezo pia wa kutwaa makombe makubwa kama lile ya Kagame," alisema Kihamia

Mwenyekiti huyo wa zamani wa kamati ya ufundi ya tawi la Uhuru na Katibu wa Yanga Bomba, Dar es Salaam alisema pia pongezi ziwaendee viongozi na benchi nzima la timu hiyo kwani hao kwa kiasi kikubwa wamefanikisha ubingwa huo.

Alisema kazi bado haijamalizika mpaka pale timu hiyo itakapofanikiwa kumfunga Simba ili kulipa kisasi cha  kufungwa mabao 5-0 katika mechi iliyopita.

No comments:

Post a Comment