Na Asha Kigundula
WACHEZAJI 25 kati ya 30 walioitwa na Kocha Kim Poulsen kwenye kikosi cha pili cha Taifa Stars (Young Taifa Stars) wameripoti kambini ambapo mazoezi yalianza tangu juzi jioni (Mei 2 mwaka huu).
![]() |
| Kocha Kim Poulsen |
Wachezaji watano walioshindwa kujiunga katika kambi ya timu hiyo iliyoko hoteli ya Sapphire jijini Dar es Salaam ni Aishi Manula, David Mwantika, Himid Mao, Samih Nuhu na Seif Abdallah ambao wako Morocco na timu yao ya Azam.
Kikosi hicho ambacho kina wachezaji wengi vijana, kitakuwa kikiitwa kambini kufanya mazoezi ya pamoja na baadhi hiyo kupandishwa Taifa Stars inayoshiriki michuano ya mchujo ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia.
Miongoni mwa wachezaji walioitwa yupo kipa namba moja ya Yanga, Ally Mustapher Barthez, wengine ni wachezaji wa Simba kutoka katika timu ya Vijana ambao ni Edward Christopher, Haruni Chanongo na Miraji Adam.





No comments:
Post a Comment