Gadget
RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA GATI NAMBA 2 KATIKA BANDARI YA MTWARA PIA AFUNGUA JENGO LA KITUO CHA KIBIASHARA CHA BENKI YA NMB MTWARA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta kitambaa pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika Ujenzi wa Gati namba mbili litakayojengwa katika Bandari ya Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania Mhandisi Deusdedit Kakoko kuhusu eneo ambalo Bandari ya Mtwara walikuwa wakilihitaji kutoka sehemu nyingine.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania Mhandisi Deusdedit Kakoko kuhusu eneo ambalo Bandari ya Mtwara walikuwa wakilihitaji kutoka sehemu nyingine.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Newala George Huruma Mkuchika mara baada ya kuwasili katika eneo la Bandari ya Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango Mtkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Ineke Bussemaker wakikata utepe kuashiaria ufunguzi rasmi wa Kituo cha Biashara cha Benki hiyo mkoani Mtwara
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Mbunge wa Mtama Nape Nnauye kuhusu ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mnolela ambapo pia amechangia kiasi cha Shilingi milioni 15 na akamuagiza Mbunge huyo kuchangia Shilingi milioni 10 kutoka fedha za jimbo.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM na Mbunge mteule wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete akifUatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati aliposimamishwa njiani na Wanakijiji wa Madangwa katika jimbo la Mtama mkoani Lindi. PICHA NA IKULU
WANAMTANDAO WA DAWA ZA KULEVYA WABUNIFU WA KILA NJIA ZA KUSAMBAZA – KAMISHINA SIANGA
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini,Rogers Sianga amesema kuwa vita ya kupambana na dawa za kulevya ni kubwa kutokana na kila siku watu wanabuni njia mpya.
Vita ya dawa za kulevya sio lelema kutokana na kuwa watu ambao wana mbinu nyingi za kufanya hivyo, lakini watakamatwa wote na hatuingii kichwa kichwa katika kufanya kazi hiyo.
Akizungumza leo katika hafla ya Timu ya Vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) kutembelea kituo cha watu walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya (Sober House) kilichopo Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
“Watu watano tumewakamta na mmojawapo aliyekuwa anasambaza dawa za kulevya Tanzania Bara na Zanzibar na jumla zaidi watu 11000 wamekamatwa ’’amesema Sianga.
Sianga amesema mtandao wote unaofanya biashara ya dawa za kulevya wameukamata, na wanaendelea kupokea taarifa mbalimbali za kuweza kutokomeza mtandao wa kuingiza dawa hizo.
Amesema wanatumia njia tatu katika kupata taarifa za watu wanaofanya biashara hiyo moja ni taarifa za watu za moja kwa moja ya pili utafiti pamoja wananchi.
Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini,Rogers Siangaakizungumza katika hafla ya timu ya Serengeti Boys chini ya miaka 17 kutembelea kituo cha watu waliodhirika na matumizi ya dawa za kulevya (Sober Hoouse)kilichopo Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani jana.
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum akizungumza katika hafla Timu ya Vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) kutembelea kituo cha watu walioadhirika na matumizi ya dawa za kulevya (Sober Hoouse)kilichopo Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani juu ya viongozi wa dini walivyo mstari wa mbele katika kupambana na dawa za kulevya.
Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini,Rogers Siangaakimkabidhi cheti , Rais wa TFF, Jamal Malizi katika hafla Timu ya Vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) kutembelea kituo cha watu walioadhirika na matumizi ya dawa za kulevya (Sober Hoouse)kilichopo Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini,Rogers Sianga akimkabidhi cheti , Mwakilishi Michuzi Media Group,Emmanuel Massaka katika hafla ya Timu ya Vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) kutembelea kituo cha watu waliodhirika na matumizi ya dawa za kulevya (Sober House)kilichopo Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Wadau mbalimbali.
SAFARI YA BAISKELI KUTOKA MBEYA KWENDA CHUNYA YADUMISHA UTALII WA NDANI NAKUTAMBULISHA RASMI MCHEZO WA BAISKELI MKOANI MBEYA
Safari hii iliandaliwa na Asasi mbili za Uyole Cultural Tourism Enterprises na ELIMISHA kwa ushirikiano na Chama cha waendesha baiskeli Mkoa wa Mbeya na Afisa Utamaduni wa Mkoa Bw.George Mbijima.
Awali, akiongea na wapenzi wa mchezo wa baiskeli,viongozi wa serikali na wanahabari
Awali, wakati wa kuwaaga waendesha baiskeli Makamu mwenyekiti wa Chama hicho Bw.Elias Mwasandele amewashukuru wadau mbalimbali wanaoendelea kuwaunga mkono zaidi sana Uyole Cultural Tourism na ELIMISHA kwa kufanikisha jambo hilo.
Aidha,kwa kushirikiana na mhazini wake wa mkoa Bw.Lucas Mhagama wameutanabaisha umma kujiunga na mchezo huo kwani ni mzuri na una maslahi mazuri kwa mchezaji na Taifa kwa ujumla.
"....kama Mkoa wa Mbeya tumebahatika kupata mwaliko wa kupeleka wachezaji wanne kwenye mashindano ya baiskeli yatakayofanyika baadaye mwaka huu nchini Afrika ya Kusini...."Bw.Mwasandele alisikika akisema.
Baada ya kupata baraka zote za mkoa kutoka kwa Afisa Utamaduni Bw.George Mbijima aliyewaasa wachezaji kuimarisha umoja,upendo na mshikamano muda wote wa safari.
Waendesha baiskeli wafuatao walisafiri kutoka Mbeya Mjini hadi Wilayani Chunya umbali wa Kilomita 70, Tumejumuisha na muda waliotumia kufika:
1.Ipyana Mbogela-Saa 2:15
2.Elias Zawadi-Saa 2:17
3.Diego Fumbo-Saa 2:28
4.Moses Mwadonde-Saa 2:34
5.Daudi Selemani-Saa 2:56
6.Kianji Samson-Saa 2:59
Hata hivyo wachezaji wawili walishindwa kumaliza safari hiyo kutokana na matatizo yaliyojitokeza kwa baiskeli zao kupata pancha wakiwa wamebakiza Kilomita 10 kumaliza safari nao ni Kristola Senga na Pasia Tanganyika.
Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Mbeya Bw.George Mbijima (wa katikati aliyevaa tracksuit ya Taifa) akiwa katika picha ya pamoja na waendesha baiskeli pamoja na viongozi wengine waandamizi kutoka Uyole Cultural Tourism Enterprises na Elimisha kabla ya safari ya kuelekea Chunya
Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Mbeya Bw.George Mbijima akizungumza na waendesha baiskeli,viongozi na wananchi katika eneo la Rift Valley wakati akiwaaga waendesha baiskeli
Waendesha baiskeli wakiingia Wilayani Chunya baada ya kumaliza Kilomita 70 kutokea Mbeya Mjini.
SUNDAY, MARCH 05, 2017 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG ~ MTUMIE RAFIKI YAKO , MAONI: 0
SUNDAY, MARCH 05, 2017
FM ACADEMIA YAKONGA NYOYO ZA WAKAZI WA KIMARA BARUTI NA MITAA YAKE
Wanenguaji na wanamuziki wa bendi ya Fm Academia wakitumbuiza katika onyesho lao lililofanyika katika Bar ya Hawa II kimara baruti jijini Dar es Salaam
Safu ya uimbaji ya bendi ya Fma Academia ikiongozwa na Rais wa Bendi hiyo, Nyoshi El Sadat wakiimba katika shoo yao ndani ya Bar ya Hawa II Kimara Baruti jijini Dar es Salaam
Malu Stonch na Partcho Mwamba wakiimba katika onesho lao lililofanyika katika ukumbi wa Hawa II Kimara jijini Dar es Salaam
Mpiga Drum akionyesha umahiri wake wa kupiga vyombo hivyo mbele ya Mashabiki wa Kimara Baruti Dar es Salaam
Wanamuziki wa Bendi ya Fm Academia wakionyesha umahiri wao wa kutawala jukwaa mbele ya Mashabiki
SUNDAY, MARCH 05, 2017
RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA JENGO LA OFISI YA BENKI KUU (BOT) PAMOJA NA NYUMBA ZA NHC MKOANI MTWARA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Beno Ndulu, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Jengo la Ofisi ya kutoa Huduma za Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi kabla ya kufungua rasmi Jengo la Ofisi ya kutoa Huduma za Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Beno Ndulu mara baada ya kufungua jengo la Ofisi ya kutoa Huduma za Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na baadhi ya watoto mkoani Mtwara waliomfata kumsalimia mara baada ya kufungua jengo la Ofisi ya kutoa Huduma za Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe kuashiria ufunguzi wa Nyumba za Shirika la nyumba la Taifa NHC katika eneo la Raha leo mkoani Mtwara. Wengine katika Picha ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa NHC Nehemia Mchechu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mbunge wa Mtwara mjini kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Maftah Nachuma kabla ya kufungua rasmi Nyumba za Shirika la nyumba la Taifa NHC katika eneo la Raha leo mkoani Mtwara.
Sehemu ya Nyumba hizo za Gorofa za Shirika la Nyumba la Taifa NHC katika eneo la Raha Leo mkoani Mtwara. PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment