NA MWANDISHI WETU
KAMPUNI ya Mawasiliano ya simu ya Mkononi, nchini Airtel Tanzania, katika msimu wa Sikukuu ya Christmass imekuja na zawadi kwa watumiaji wa mtandao huo kupitia promosheni inayoitwa MR. Santa.
Ambapo mteja na mtumiaji wa mtandao wa Airtel ili aweze kuingia kwenye kinyang'anyilo cha Mr. Santa anapaswa kufanya miamala mbalimbali ikiwemo kutuma na kupokea pesa.
Hayo yamebainishwa leo Desemba 20 jijini Dar es Salaam na Meneja mahusiano wa Kampuni hiyo, Jackson Mmbando, amesema droo ya promosheni hiyo itakuwa ikiwawezesha watumiaji wa mtandao huo kujipatia zawadi kem kem ikiwemo, fedha tasilimu na vitu vya thamani kama luninga, pikipiki , mbuzi , Smart fone za kijanja.
" Hakikisheni wateja wetu wa Airtel mnafanya miamala wiki hii kwa ajili ya Sikukuu ya Christmass kwa kutuma na kupokea pesa, kulipia bili mbalimbali utaweza kujishindia na kujipatia zawadi kutoka kwa mr. Santa," amesema Mmbando.
Aidha ameongeza kuwa mtandao wa Airtel unawataka watumiaji wake wakiwemo mawakala, wapenzi kufanya miamala hiyo mara moja kwa wiki hususan siku ya Jumanne ya wiki, ambapo itakuwa inatoa washindi mbalimbali watakuwa waliofanya miamala hiyo.
Ameongeza kuwa Promosheni ya Airtel Santa Mizawadi inalenga kuwashukuru wateja na mawakala waaminifu na wanaoendelea kutumia Airtel katika msimu wote huu wa Sikukuu.
“ Airtel Santa Mizawadi ni promosheni kabambe ambayo itawapa washindi fursa ya kuondoka na zawadi kemkem ikiwemo pocket WiFi, simu janja, pikipiki, runinga na pesa Taslim" amesema Mmbando.
Akielezea jinsi ya kushiriki na kujishindia Mizawadi ya Airtel Santa Mizawadi, Mmbando amesema Kwa Wakala wa Airtel anatakiwa kufanya miamala ya kuweka na kutoa fedha na Kwa mteja anachotakiwa kufanya kununua bando, kulipa bili, kutuma na kutoa fedha, kununua muda wa maongezia au vifurushi kupitia *149*99#, *150*60# au kupitia 'My Airtel App'.
Kwa upande wake Meneja Huduma Kwa Wateja ,Celina Njuju amesema Mr. Mazawadi yupo pamoja na watumiaji wa mtandao wa Airtel na unawathamini wateja wake ambapo Mr. Santa atakuwa akizunguka maeneo mbalimbali nchini kuhakikisha huduma za Airtel zinawafikia wengi ipasavyo.
Hata hivyo droo itakuwa ikichezeshwa mara moja kwa wiki na mshindi atakuwa akipigiwa simu kwa kutumia namba 100 pekee na kuambiwa aina ya zawadi aliyojishindia.
Naye msanii maarufu, Lucas Mhavile," Joti' ambaye ndio amekula shavu la Mr. Santa amesema kuwa msimu huu wa sikukuu Airtel inawajali wateja wake kwa kutoa zawadi Kem Kem kwa kufanya miamala mbalimbali kwa kulipia bili, kutuma na kupokea pesa, nunua cho chote ambapo unajitengenezea nafasi kubwa ya kupata zawadi.
Nae msanii maarufu Lucas Mhavile 'Joti' katika Promosheni hiyo ndio Mr. Santa amesema kuwa msimu huu wa Sikukuu, Airtel inawajali wateja wake kwa kutoa zawadi kem kem kwa wale watakaofanya miamala mbalimbali kwa kulipia bili, kutuma na kupokea pesa, kununua chochote ambapo unajitengenezea nafasi kubwa ya kupata zawadi.
No comments:
Post a Comment