JIWE LA MSINGI LAWEKWA UWANJA WA BANDARI DAR - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, March 4, 2017

JIWE LA MSINGI LAWEKWA UWANJA WA BANDARI DAR

Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing akizungumza katika hafla yauwekaji wa jiwe msingi kuanza ujenzi wa kiwanja cha Bandari ambacho kitagharimu Dola za Kimarekani 450,000, jana jijni Dar e Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwa kushirikiana na Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing wakiweka jiwe la msingi kuanza ujenzi wa kiwanja cha Bandari ambacho kitagharimu Dola za Kimarekani 450,000,jana jijni Dar e Salaam.
Baadhi ya wananchi wakishuhudia uwekaji wa jiwe la msingi la kuanza ujenzi wa kiwanja cha Bandari ambacho kitagharimu Dola za Kimarekani 450,000, jana jijni Dar e Salaam.
Katibu Tawala Manispaa ya Temeke, Hashim Komba akizungumza machache  katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la kuanza ujenzi wa kiwanja cha Bandari


Ikiwa imepita miezi kadhaa tangu Balozi kukubaliana na ombi la Mkuu wa Mkoa, leo tarehe 3 Balozi huyo wa China akiwa na RC Makonda wameweka historia mpya baada ya kuweka jiwe la msingi la kuanza ujenzi wa viwanja hivyo, huku wakianza na kiwanja cha Bandari ambacho kitagharimu Dola za Kimarekani 450,000,

Huku kikijengwa kwa viwango vya kimataifa na kampuni iliyojenga uwanja wetu wa taifa. Kuonyesha na kutambua utendaji na msukumo mkubwa wa RC Makonda katika kutimiza azma ya Rais John Pombe Magufuli ya kutatua changamoto za wanyonge, Balozi pia amemuahidi Mkuu wa Mkoa kutoa kipaumbele cha ajira vijana wote watakaoshiriki mashindano ya Ndondo Cup kwenye kampuni mbili ambao watakuwa vijana zaidi ya 20000.

No comments:

Post a Comment