WAFANYAKAZI WA ZANTEL WACHANGIA DAMU KUSAIDIA WENYE MAHITAJI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, March 1, 2017

WAFANYAKAZI WA ZANTEL WACHANGIA DAMU KUSAIDIA WENYE MAHITAJI

Akizungumza wakati wa mchakato huo  wa damu lililofanyika kwenye makao makuu ya ofisi za Zantel jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma, kwa niaba ya Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu Zantel, Bw. Frank Jackson alisema kwamba juhudi hizo zilianzishwa ili kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili wagonjwa wengi wenye uhitaji wa kuongezewa damu hapa nchini huku lengo pia likiwa ni kuokoa maisha ya wananchi kadri inavyowezekana hususani wakina mama pamoja na watoto walio chini ya miaka mitano.
“Tunayofuraha isiyo kifani kwa kukamilisha shughuli hii leo, ambayo kimsingi inaonyesha uhusiano na wajibu wetu kwa jamii lengo letu likiwa ni kuhimarisha afya za Watanzania wenzetu,” alisema Bw. Jackson.
Aliongeza kuwa, katika nchi zenye watu wengi wenye kipato cha chini watoto walio chini ya umri wa miaka mitano wanahitaji siyo chini ya asilimia 65 ya damu yote inayochangiwa kila mwaka ili kuokoa maisha yao.
“Sisi kama kampuni tumeona ni wajibu wetu kushiriki katika zoezi hili la uchangiaji damu ili kuendelea kuokoa maisha ya wananchi,” alisema.
Kwa upande wake mwakilishi kutoka Mpango wa Taifa wa damu Salama-Kanda ya Mashariki, Bi. Fatuma Mjungu alisema, “Tumefurahi sana kuungana na baadhi ya wafanyakazi wa Zantel leo katika kufanikisha zoezi hili ambalo linahitaji uhamasishaji mkubwa. Tumefurahishwa zaidi na mchango mkubwa ulioonyeshwa  na timu ya Zantel ambayo imethibitisha wazi kwa jinsi walivyokuwa tayari kujitolea katika kusaidia Watanzania”.
Aliongeza kuwa mahitaji ya damu nchini bado ni makubwa na bado wanahitaji ushirikiano kutoka kwa watu mbalimbali ili kuweza kufikia lengo la kukusanya lita 300,000 zinazohitajika kila mwaka ili kuwahudumia watu wenye mahitaji ya huduma hiyo.

No comments:

Post a Comment